Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 21 August 2015

POMBE KIDOGO PIA YAWEZA KULETA MADHARA

Unywaji kidogo wa pombe hadi chupa moja kwa siku kwa wanawake na chupa mbili kwa wanaume unaweza kusababisha hatari ya kupata saratani kulingana na watafiti.
Makala moja ya Uingereza ilichambua utafiti mkubwa kutoka nchini Marekani uliofanyiwa zaidi ya watu 100,000.
Wataalamu wanasema kuwa matokeo hayo yanatuma ujumbe wa kiafya kuwa watu wanahitaji kupunguza kiwango cha pombe wanachokunywa na mara nyinge hata kuwa na siku ambazo hawanywi pombe.

Pombe kidogo pia yaweza kuleta saratani

Mara nyingi inahitajika kuwa wanaume wanaweza kunywa zaidi ya chupa tatu kwa siku na wanawake zaidi ya chupa mbili au tatu lakini huenda viwango hivyo vikafanyiwa marekebisho.
Watafiti hao pia waligundua kuwa hatari inayotoka na unywaji wa pombe hasa satarani ya matiti iliongezeka hata kwa kunywa chupa moja ya pombe kwa siku.
BBC

No comments:

Post a Comment