Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 16 August 2015

NTIMIZI: NIMETUKANWA, NIMEDHALILISHWA MUNGU ALIKUWA NAMI

Mussa Ntimizi


Na Hastin Liumba, Uyui 
KADA wa chama cha mapinduzi (CCM) aliyepitishwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu mwezi oktoba 25,mwaka huu Musa Ntimizi, amesema licha kutukanwa na kudhalilishwa Mungu amempigania amepita kugombea ubunge jimbo la Igalula.
Hata hivyo Ntimizi aliwaomba wanaCCM wenzake ambao wamepitishwa na vikao vya juu kugombea kwenye nafasi za udiwani na Ubunge waache kushangilia sana na kunyanyapaa walioshindwa.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa mapokezi yake katika kata ya Kigwa na baadaye Igalula ambapo alitoa hotuba fupi ya kushukuru kupata fursa hiyo.

Alisema kwa sasa sioni sababu ya waliopitishwa kushangilia ana kuanza kutukana wengine walioshindwa hizo siyo siasa bali ni kutaka kuendekeza makundi CCM ni yetu sote.

Alisema hana moyo wa kinyongo kwani katika kura ya maoni alikumbana na vikwazo vingi ikiwemo kesi,vijarida na vipeperushi vya kumchafua lakini Mungu alisimama imara na hatimaye ameshinda.

Alisema licha ya hayo anawasamehe wote waliofanya hayo na sasa anaanza upya kazi ya kujipanga kutetea jimbo hilo mbele ya wapinzani (UKAWA).

‘Niko radhi kushirikiana na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dk Athuman Mfutakamba na Hanifa Kitwanakondo ….hawa nilipambana nao kwenye kura ya maoni.”alisema.

Ntimizi alisema haoni sababu ya kuwa na makundi baada ya kumalizika vikao vya uteuzi na hii ni kwa faida ya nani wakati wananchi wanahitaji maendeleo.

Alisema ni kweli ameshinda ambapo katika kata 11 ameshinda kata saba (7) hivyo ni dhahiri kuwa wanancghi wanamuhitaji hivyo hatawaangusha.

Alisema anawashukuru wote waliomchagua na wasiomchagua na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli lakini nisingependa walioshindwa waanze kunyanyapaliwa si vyema.

Alisema anajua ugumu wa kuvunja makundi ndani ya  vyama lakini inabidi kufanya hivyo kama kweli tunataka kushinda uchaguzi wa mwezi oktoba 25,mwaka huu.

Ntimizi anatarajia kuchukua fomu ya kugombea uchaguzi siku ya jumanne.

No comments:

Post a Comment