
Dk. Raphael Chegeni.
Busega .Hatimaye kitendawili kilichokuwa kikisubuliwa kwa hamu na wananchi wa jimbo la Busega mkoani Simiyu, kimeteguliwa baada ya kamati ya siasa ya wilaya hiyo kumtangaza Dk Raphael Chegeni kuwa mshindi katika kura za maoni ndani ya chama.
Matokeo hayo yamekuja baada ya Kamati Kuu ya CCM kuagiza uchaguzi huo kurudiwa kwa kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu, huku wagombea wote wakilalamikia vitendo vya rushwa katika matawi na vituo vya kupigia kura.
Akitangaza matokeo hayo kaimu katibu wa CCM wa Busega, ambaye pia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Jonathan Mabia alimtangaza Dk Chegeni kuwa mshidi baada ya kupata kura 13,838 akifuatiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani aliyepata kura 11558.
Mabia alisema jumla ya wapiga kura 28,127 walijitokeza kupiga kura, lakini kura 457 ziliharibika na kubaki kura halali 27,700.
Dk Chegeni ambaye ndiye mshindi wa kura za maoni ya ubunge wa jimbo la Busega, akizungumzia matokeo hayo alisema hiyo imetokana na ufuatiliaji wake wa kuhoji viashiria vya udanganyifu wa matokeo alivyoviona.
Alisema makundi ndani ya CCM katika wilaya hiyo yaweza kukifikisha pabaya chama kutokana na baadhi ya viongozi kuwabeba wagombea, na kwamba kwa ushindi huo ni bora wakaunga kuhakikisha wanapata ishindi kwenye uchaguzi mkuu.
Kwa upande wake Dk Titus Kmani alionyeshwa kutokulidhishwa na matokeo hayo, na kudai kuwa matokeo aliyopata Dk Chegeni ni uhuni uliofanywa na baadhi ya wapambe wake wa kubadilisha matokeo katika vituo.
“Nimefika kwenye ofisi ya chama asubuhi ili kuweza kuingia katika chumba cha kuhesabia matokeo, cha kushangaza kamati ya siasa ilijifungia na mmoja wa wagombea hao ambaye hapa sasa wamemtanga mshindi, inaonyehsa ni dhahili kweli matokeo hayo wametengeneza,” alisema Dk Kamani.
CREDIT: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment