Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 13 August 2015

ETI SAID NKUMBA HAJAMUAGA BABA YAKE KWENDA CHADEMA!

Mwalimu Said Nkumba

Na Hastin Liumba, TaboraALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora Said Nkumba amesema wakati anaondoka CCM na kujiunga na CHADEMA hakumwambia mzee Juma Nkumba ambaye ni baba yake mzazi.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akijiunga na CHADEMA baada ya kudai kwa kile alichofanyiwa na viongozi wa CCM kwenye kura za maoni.

Alisema amejiunga na CHADEMA bila kumwambia baba yake mzazi Juma Nkumba ambaye ni mwasisi wa TANU na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora.

Alisema CCM aliipenda sana lakini kutokana rafu za viongozi wenye dhamana kufanya ndivyo sivyo ameona chama hicho sasa ni dhahiri hakifai.

Alisema siyo rafu tu ndizo zimemkimbiza bali hata misingi ya CCM sasa imekufa na kilichobaki ndani ya chama hicho ni fedha tu bila fedha huna nafasi ndani ya CCM.

“Mabadiliko ni sasa na mabadiliko hayo siyo ndani ya CCM ni nje ya chama hicho nikimmanisha CHADEMA”.alisema.

Alisema ameandaa mkutano mkubwa Sikonge na atakwenda kuwaomba radhi wananchi kabla ya kuwaomba kuondoka CCM ili aungane nao.

Aliesema atawaambia madhambi ya CCMkwani wakati yuko ndani ya chama hicho alikuwa akishindwa kusema uozo hivyo sasa kapata nafasi.

Kuhusu tumbaku sasa ana ukweli ulivyo jinsi baadhi ya viongozi wa CCM walivyoibia wakulima hao na ataanika kila kitu.

Nkumba alisema ameutua mzigo wa kuulizwa maswali na wakulima wa tumbaku kilichobaki ni kupambana ili mkulima wa zao hilo anufaike.

“Nilikuwa nikulizwa maswali mengi na wakulima wa tumbaku lakini nilikuwa napindisha ukweli kwani nilikuwa nipo ndani ya CCM na wakati mwingine nikiwa kitandani nawaza na Napata wakati mgumu kwa aibu kwani nilipindisha ukweli”.alisema.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi alipoulizwa kuhusu kutuhumiwa uongozi wa chama hicho mkoa na wilaya alisema hawezi kujibu malumbano.

No comments:

Post a Comment