Marehemu Emeneya anasifika kwa kuanzisha utumizi wa zana za elektroni katika muziki nchini DRC.
Watu kadhaa
wameripotiwa kufariki baada ya kutokea mkanyagano katika tamasha la kumkumbuka
mwanamuziki maarufu wa Congo King Kester Emeneya.
Baadhi ya vyombo vya
habari vinasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki ingawa maafisa wakuu bado
hawajatoa takwimu rasmi za watu.
Maafisa wanasema kuwa
mwanamuziki huyo alifariki mjini Paris mapema mwaka huu akiwa na umri wa miaka
57.
Idadi kubwa ya watu
ilikusanyika nyumbani kwake mjini Kikwit katika Jamhuri ya kidemokrasia kwa
tamasha hilo la kumkumbuka.
Maelfu walihudhuria
mazishi ya marehemu nyumbani kwake karibu na mji wa Kinshasa mwezi Machi baada
ya kifo chake mwezi Februari kutokana na maradhi ya Moyo.
Shirika la habari la
AFP limesema kuwa Emeneya alikuwa mwanamziki mbunifu aliyeanzisha utumizi wa
zana za kielektroniki katika muziki nchini Congo.
Tamasha hilo
lililotarajiwa kuendelea hadi Jumapili limefutiliwa mbali.
CHANZO BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment