Watoto wa kituo cha Amani Orphanage Centre wakifurahia baadhi ya vifaa vilivyotolewa na TAS.
Chama cha Watanzania
waishio Geneva wametoa mchango wa vifaa ikiwa
pamoja na tank la kuhifadhia maji,viti
na meza za kusomea, jiko la gesi na mtungi wa Gesi ili kusaidia watoto wa kituo
cha Amani Orphanage Centre. Msaada huo uliwasilishwa kwa niaba ya TAS na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt Agnes Kijazi. Akiwasilisha mchango huo kwa niaba ya TAS, Dkt
Kijazi alielezea upendo walionao watanzania hao kwa kuwakumbuka watoto wa kituo cha Amani. Alisema
upendo huo ni mfano wa kuigwa kwa watanzania waishio ndani na nje ya nchi. Kwa
upande wa watoto Dkt. Kijazi aliwahakikishia kwamba TAS na TMA wanawapenda. Alichukua fursa hiyo
kuwakumbusha upendo ambao umeonyeshwa kwao na wanawake wa TMA kwa kuwasaidia
baadhi ya mahitaji yao.
Aidha Dkt Kijazi alisema TAS wameendelea kuonyesha moyo wa upendo kwani
hivi karibuni wametoa msaada wa fedha (Tshs 500,000) kwa Mama Aida wa Mbeya
aliyejifungua wototo wanne mwanzoni mwa mwaka huu. Msaada huo uliwasilishwa kwa
niaba ya TAS na meneja wa TMA kanda ya nyanda za juu kusini magharibi Bwana
Issa Hamad.
Akipokea msaada huo
msimamizi na mwanzilishi wa kituo cha Amani Bi. Margareth Mwegalawa aliwashukuru watanzania wote waishio Geneva
kwa kuwakumbuka watoto wa Amani hata kuwawezesha kupata baadhi ya mahitaji
waliokuwa wanahitaji, na alimuomba Dkt Kijazi kuwasilisha salamu hizo kwa
kusisitiza msaada huo sio mdogo bali ni mkubwa sana kulingana na uhitaji wake. Bi.
Magreth alisema kituo chicho kina watoto 37 wakiwa wasichana 25 na wavulana 12
wenye umri kati ya mwaka mmoja (1) na miaka kumi na tano (15).
Akizungumza kwa niaba
ya watoto wa Amani Orphanage Centre mtoto Beatrice Phine alisema sote
tunafurahi kwa kupata tank la maji, viti na meza ambavyo vitaboresha maisha
yetu na mazingira ya kusomea. Alimuomba Dr. Kijazi awafikishie salaam zao za
upendo na shukrani kwa TAS.
Picha Na 1
Picha Na 2
Picha Na 3
Meneja wa TMA Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini magharibi Bw. Issa Hamad akikabidhi msaada kwa mama wa
watoto mapacha wanne kwa niaba ya TAS
No comments:
Post a Comment