Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 26 April 2014

VIPI UZINDUZI WA KATIBA MPYA APRILI 26, 2014?


Ndugu zangu,
Bunge Maalum la Katiba limeahirishwa jana Ijumaa Aprili 25, 2014 lakini likiwa halijamaliza hata kujadili sura mbili, tena bila kuwepo kwa wajumbe 201 wanaounda kundi la UKAWA.
Asilimia kubwa ya wajumbe hao ni wale wa vyama vya upinzani, ambao wamesisitiza kwamba kamwe hawatarudi Bungeni kwa madai kwamba Chama cha Mapinduzi kina nia mbaya hasa katika suala la muundo wa Serikali.
Bunge hilo, kwa mujibu wa taaria, linaweza kuendelea baada ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti ambalo litaanza mwezi Mei.
Lakini itakumbukwa kwamba, mnamo Jumamosi Juni 25, 2011 Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema mjini Dodoma kwamba Katiba Mpya ingezinduliwa leo Aprili 26, 2014.
Waziri Mkuu Pinda alitoa kauli hiyo wakati akizindua Semina Elekezi kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper.
Kwa mnyukano tulioushuhudia mjini Dodoma hivi karibuni, bado kuna mashaka ni lini Katiba Mpya itapatikana na hatimaye kuzinduliwa, kwa sababu mbali ya mjadala wa Bungeni, lakini pia bado kuna Kura ya Maoni ya Wananchi ambayo inatakiwa iendeshwe nchi nzima.
Na hii hapa chini diyo taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu kuzinduliwa kwa Katiba Mpya Aprili 26, 2014:

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

KATIBA MPYA ambayo mchakato wake umeanza inatarajiwa iwe imekamilika na kuzinduliwa rasmi Aprili 26, 2014 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema mjini Dodoma leo *(Jumamosi Juni 25, 2011)*.

Akifungua Semina Elekezi kwa Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper, alisema hayo ndiyo matarajio ya Serikali.

“Ni matarajio ya Serikali kuwa Katiba Mpya itakuwa imekamilika na kuzinduliwa ifikapo tarehe 26 Aprili, 2014 katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kwamba kama mambo yote yatakwenda kama yalivyopangwa, Muswada wa Sheria kuhusu Mapitio ya Marekebisho ya Katiba utawasilisha Bungeni mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge unaoendelea hivi sasa au mwanzoni mwa Mkutano wa Tano Oktoba mwaka huu.

Aliwataka Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kutoa ushirikino wa kutosha kwa Tume ya Kuratibu na Kusanya Maoni itakayoundwa ili kuwezesha mikutano ya hadhara ya kukusanya maoni kufanyika kama ilivyokusudiwa kwa kuhamasisha wananchi kuhudhuria na kutoa maoni yao.

“Katika suala hili kubwa nala kitaifa, ni vyema viongozi wasiingize siasa na wajiepushe kuwashawishi Wananchi katika kutoa maoni yao, bali wawaache watoe maoni kwa uhuru au pasipo shinikizo lolote,” alisema.

Mchakato huo wa kuelekea uundwaji wa Katiba Mpya, umekwishaanza na katika hatua ya awali, Serikali imeandaa rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba *(The Constitutional Review Act*) ya Mwaka 2011.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa hatua ya sasa siyo kutunga Katiba Mpya bali ni kuunda Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuelekea kutungwa kwa Katiba Mpya.

(mwisho)

*Imetolewa na:*

* Ofisi ya Waziri Mkuu,*
* S.L.P. 980,*
* DODOMA*

*Jumamosi Juni 25, 2011*


No comments:

Post a Comment