Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 21 April 2014

NENO LA HEKIMA: TUSIWAAMINI WATU

Ndugu zangu,
Wanadamu wanabadilika. Hawatabiriki. Wapo wanaobadilika kutokana na hali ya maisha. Hawa daima wanaweza kuwa katika hali fulani ya maisha. Wengi wao ni wenzangu na miye, ambao wako katika ama hali duni au za kawaida, ambao hata mwenendo wao unakuwa wa kawaida wakati wanapokuwa hawana kitu.
Lakini kadiri neema inavyowajilia ndivyo ambavyo wanabadilika tabia. Kama mlikuwa mnapiga story hata kijiweni, mkicheza wote bao, lakini mambo yanapowanyookea wanaweza hata wasiwapungie mkono. Wengine wanaweza kubadilika kwa tamaa tu. Hawa unaweza kuwashauri wakaacha tabia hiyo.
Lakini kuna hawa wengine ambao ni hulka yao. Si mnatambua kwamba hulka huwa haibadiliki? Iko kama ngozi, hata uweke mkorogoro kamwe haiwezi kuonekana kuwa ya asili.
Basi hawa ndio majanga makubwa katika jamii. Anapokuwa katika hali fulani huwezi kuitambua hulka yake, lakini mara mambo yanapomnyookea utaiona hulka yake. Kama ni mlafi utamuona, kama ni mnafiki utamjua, na mambo mengine kadha wa kadha.
Hata kama mmekubaliana jambo fulani, lakini mambo yanapokuwa yamenyooka watu hawa hubadilika ghafla na ndipo utakapoona ulafi wao, unafiki wao, uchoyo wao na hila zao chafu. Hakika hawa ni wa kuogopwa. Daima utawakuta watu hawa kwenye macho ya jamii kama ni wema, maneno yao yanaonekana ya busara sana. Wakati mwingine unaweza kudhani wanastahili kuwa mahali pa juu zaidi kuliko walipo sasa. Lakini, maskini weee, ukiwachunguza hulka zao ndipo utakapogundua kwamba hata hapo walipo hawastahili. Wema wanaojaribu kuuonyesha kwa jamii ni unafiki uliopindukia. Hawafai hata kupewa nafasi ya kuchunga kuku.
Tujihadhari nao, wapo katika jamii yetu hawa.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega

No comments:

Post a Comment