wanamgambo wanaeondelea kuyadhibiti majengo ya serikali mashariki mwa Ukraine.
Viongozi wa nchi zenye
uwezo mkubwa duniani G7 wamekubaliana kuiwekea vikwazo zaidi Urusi, wanayosema
inaendelea kuchochea ghasia mashariki mwa Ukraine.
katika taarifa yao,
viongozi hao walionyesha wasiwasi wao kuhusu jitihada za wanaharakati wanaounga
mkono Urusi kuendelea kuyumbisha mashariki mwa Ukraine.
Urusi ,wamesema
haijachukua hatua zozote kutekeleza makubaliano ya mjini Geneva mbali na
kuwaamrisha wanamgambo hao kuondoka katika majengo ya serikali wanayodhibiti.
Hatahivyo viongozi hao
wameipongeza Ukraine kwa kujizuia katika kukabiliana na makundi ya wanamgambo
yaliojihami.
Wakati huohuo,
wanamgambo wanaounga mkono Urusi mashariki mwa mji wa Ukraine wa Slavianski
wamelitekanyara kundi moja la wachunguzi 13 wa kimataifa pamoja na wale wa
Ukraine ambao walikuwa wanazuru eneo hilo wakiwa miongoni mwa ujumbe
unaoshirikishwa na shirika la usalama la muungano wa Ulaya.
Kundi hilo
linashirikisha wachunguzi wa kijeshi wa Ujerumani pamoja na wawakilishi wa
Denmark,Poland,Sweden na jamhuri ya Czech.
Kiongozi mmoja
anayeunga mkono Urusi amesema kuwa wachunguzi hao wamezuiliwa kwa kuwa
mpelelezi mmoja wa serikali ya Ukraine alikuwa miongoni mwao.
Ujerumani imesema kuwa
itatumia njia zote za kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa wamewachiliwa huru.
Na huku hali ya
wasiwasi ikipanda,Marekani imesema kuwa imegundua kwamba ndege za kijeshi za
Urusi zimekuwa zikiingia katika anga ya Ukraine katika kipindi cha masaa 24
yaliopita.
CHANZO BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment