Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 19 January 2017

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MPINGO HOUSE

 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye baada ya kuwasili makao makuu ya Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam jana huku akiongozana na wajumbe wa kamati hiyo.

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 300 ZILIZOKUWA ZIENDE KWA KWA WAKANDARASI


 Image may contain: 1
person, phone and indoor


Na Woinde Shizza,Arusha
Halmashauri ya jiji la Arusha imeokoa zaidi ya shilingi  milioni mia tatu
sitini na nne  zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kuwapa wakandarasi  kwa ajili ya kujenga madarasa  baada yake  kamati za shule kupewa jukumu la kusimamia ujenzi wa madarasa hayo badala ya mkandarasi.

WAFANYABIASHARA WAILALAMIKIA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA ,WAPINGA NOTISI WALIYOPEWA

Image result for WAFANYABIASHARA WA MADUKA ARUSHA

Na Woinde Shizza, Arusha


WAFANYABIASHARA wa maduka jijini Arusha,wameilalamikia halmashauri hiyo ,wakipinga notisi ya miezi mitatu waliopewa ,inayowataka kuondoka katika maduka hayo,ifikapo Machi 30,mwaka huu, kufuatia maduka yao kudaiwa kumilikiwa ma madalali na hivyo kuikosesha  mapato halmashauri hiyo.

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA ELIMU KWA WADAU KUHUSU UALIBINO JIJINI MWANZA.

Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ufunguzi wa semina kwa wadau wanaosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualibino, inayofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jijini Mwanza. 

MADIWANI WA MANISPAA YA MOSHI WATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA)

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa ukaribisho wa Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi walipotembelea ofisi za mamlaka hiyo.

WASICHANA WANNE WA TANZANIA WAENDA KUPATA MAFUNZO YA UONGOZI, UTAMADUNI AFRIKA MASHARIKI NA KATI


 Wasichana wanne wa Tanzania wakiaga  kwa kupungia mikono huku wakiwa na , Bendera ya Taifa waliyokabidhiwa na Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia ni Farida Mjoge,Elizabeth Betha, Edna Chembele na Ummy Mwabondo.

MSIMU WA 15 WA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MBIO ZA KILIMANJARO PREMIUM LAGER MARATHON 2017 WAZINDULIWA RASMI MKOANI KILIMANJARO.

Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa 15 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ,uzinduzi uliofanyika Kibo Palace Home mjini Moshi.

TANZANIA KUANZA KUTUMIA MFUMO WA DIRISHA MOJA LA HUDUMA (ELECTRONIC SINGLE WINDOW SYSTEM)

Kaimu Kamishna Mkuu TRA, Mary Maganga.
Katika kuhakikisha inaboresha huduma kwa wafanyabiashara ambao wanaingiza mizigo nchini kwa njia ya bandari, mipaka na viwanja vya ndege, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeeleza mpango wa Serikali wa kuanza kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System) ambao kwa hakika utamaliza tatizo la mizigo kukaa muda mrefu kwa sababu ya kukosekana vibali.

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA TTSA, TAWA NA TAFORI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizaya hiyo, Meja Generali Gaudence Milanzi (kushoto) wakiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipowasili katika ofisi za Wakala ya Miti za Mbegu Tanzania (TTSA) mjini Morogoro jana kwa ajili ya kuona kazi na miradi ya wakala huyo. Kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo, Silafi Maufi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa na Godwin Molel (wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Siha.

PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA POSTA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasili Ofisi za Posta Kuu ya Shirika la Posta maeneo ya Posta Mpya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

ZINGATIA HAYA ILI KUREJESHA ARI YA KUFANYA KAZI BAADA YA LIKIZO


Na Jumia Travel Tanzania

IWAPO unazitambua vizuri barabara za jiji la Dar es Salaam, basi utagundua kwamba kuna tofauti kubwa kwenye msongamano wa magari ukilinganisha na kipindi cha sikukuu. Hali hiyo imetokana na idadi kubwa ya watu kurejea jijini kuendelea na shughuli za kazi, ambapo wengi walikuwa kwenye likizo na mapumziko ya mwisho wa mwaka.

WAZIRI MKUU AONGOZA KUZINDUA DUKA LA BOHARI YA DAWA (MSD), MPANDA, MKOANI KATAVI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Dawa la Bohari ya Dawa (MSD), Mpanda mkoani Katavi. Kutoka shoto mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa  Katavi, Peter Mselemu, Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali mstaafu Raphael Muhuga. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KINGDOM LEADERSHIP NETWORKS


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School.

TIGO YAZINDUA TWENDE APP KUSAIDIA HUDUMA YA USAFIRI WA TEKSI NCHINI TANZANIA

 Mkuu wa Zana za Kidijitali wa Kampuni ya Simu ya Tigo,  Tawonga Mpore (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuzindua Twende APP kwa ajili ya kusaidia huduma ya usafiri wa teksi nchini. Kulia ni Mkuu wa Utawala na Fedha wa DTBi ambao ni wawezeshaji wa mradi huo, Mramba Makange na Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu wa Costech,  Dk. Digushilu Mafunda.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA, UKONGA JIJINI DAR

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na Mshauri wa Kitengo cha Utafiti wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BICO,UDSM), Dk. Dalmas Nyaoro, baada ya kuwasili eneo la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Magereza ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika  katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

RITA KABATI: WAPINZANI HAWATASHINDA UCHAGUZI MDOGO WA KATA YA IGOMBAVANU NA IKWEA

 

Mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati akimpigia kampeni mgombea udiwani wa kata ya Igombavanu na kuwataka wapinzani kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MAHAKAMA YA UMOJA WA MATAIFA (UNMICT-TAWI LA ARUSHA), JIJINI DAR



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo wakati viongozi wa Mahakama hiyo walipomtembelea kiongozi huyo wa Wizara, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo. Katikati ni Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Monday, 16 January 2017

VIDEO: BINTI ALIYE MDATISHA MWANAUME MTANDAONI KWA PICHA ZISIZO ZAKE AAIBISHWA

Ni jambo la kusisimua kutokana na huruka za vijana kwenye mitandao ya kijamii, hii ni mara baada ya kuona matumizi mabaya ya mitandao kama Facebook,Twitter, Instagram nk vikiongezeka. Vijana wengi  wanashindwa kutumia mitandao ya kijamii  kwa ajili ya masilahi yao badala yake wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kutafuta wapenzi,utapeli, umbeya, kuanika nyeti zao yaani kuweka picha chafu nk.

TAASISI ZA UMMA MARUFUKU KUJENGA VITUO BINAFSI VYA KUHIFADHI DATA

Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.

WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WAHAKIKIWA KIGOMA

Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akimhudumia mstaafu wakati wa zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, linalofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Kigoma, Mkoani Kigoma.