Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 24 April 2014

MLIPUKO WAUA WATU WANNE JIJINI NAIROBI

    Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza.

Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.

Kulipatikana bomu la pili katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao, usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi inaendelea kufanya uchunguzi.

Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye iituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
"kilie kingine kilinikuta kwenye kibanda changu ni nyama ya watu ilinirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje," Bwana Muigendi alisema.

Mtaalamu wa maswala ya usalama wa jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.

 Chanzo bbcswahili

No comments:

Post a Comment