Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 25 March 2015

PAN AFRICA, CHANGANYIKENI KUSAKA NAFASI YA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

Baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es Salaam na timu za FFU na Zakhem kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye makundi yao, kesho 20/03/2015 utapigwa mchezo mmoja wa kusaka nafasi ya kuungana na mabingwa hao kushiriki michuano ya ligi ya mikoa.
Mchezo huo wa mtoano utakaopigwa katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,utazikutanisha timu za Pan Africa dhidi ya Changanyikeni ambazo zimemaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi yao.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam,DRFA,baada ya kumpata mshindi katika mchezo huo, majina ya timu hizo tatu yatapelekwa shirikisho la soka la Tanzania TFF.
Aidha kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Kenny Mwaisabula,imewashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja mbalimbali kushuhudua michuano ya ligi mkoa wa Dar es salam tangu ilipoanza kutimua vumbi.

No comments:

Post a Comment