Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 25 March 2015

WACHIMBAJI WADOGO TABORA WAPATA UONGOZI

Wachimbaji wadogo

Na Hastin Liumba, Nzega
CHAMA chama cha wachimbaji wadogo  wa madini mkoa wa Tabora (TABOREMA) hatimaye  kimepata uongozi mpya.


 Chama hicho sasa kitaongozwa na mwenyekiti  wake  Rashidi  Shaout  baada ya kufariki dunia kwa aliyekuwa mwenyekiti  wa awali  Joseph  Masolwa.

AKizungumza baada ya kutangazwa mshindi  Shabout  alisema kwa muda mrefu wachimbaji   wadogo wa madini wa mkoa wa Tabora walikosa mwenyekiti wa chama hicho hali iliyopelekea kushindwa kutekeleza na kutatua matatizo ya wananchama hao kwa muda.

Alisema   kwa sasa wachimbaji wadogo watapata  fursa ya kuonana na mwenyekiti ikiwa na kutatua kero mbalimbali ambazo zilishindwa kutatuliwa kwa muda muafaka na kuongeza kuwa wachimbaji hao wanapaswa kutii sheria bila shuruti.


Aliwataka viongozi wengine wa chama hicho kuongeza ushirikiano wa utendaji kazi ikiwa na kuwatembelea wachimbaji wadogo katika migodi yao ilikubaini matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa haraka.


Alisema chama hicho kilikuwa kikikabiliwa na changamoto ya nafasi ya mwenyekiti hali iliyopelekea kushindwa kufanya kazi zake kwa  ufanisi ambapo kwa sasa kinatarajia kutatua matatizo ya wachimbaji wadogo ikiwa na kuishawishi serikali kutoa leseni za viwanja vya madini.

Mjumbe wa mkutano mkuu mkoa Maulidi  Mtumba amekitaka chama hicho kuhakikisha kinatatua matatizo ya wachimbaji kwa muda muafaka na kuutaka uongozi kutoa mafunzo mbalimbali kwa wachimbaji.

No comments:

Post a Comment