“Natumia nafasi hii kueleza juu ya maneno ambayo yalitolewa na mchungaji
fulani, sikumbuki anaitwa nani… nasema nimemsamehe kutoka ndani ya moyo
wangu wote anaweza kuwa na sababu zake ila nimemsamehe kabisa” Kardinal
Pengo
Na Kelvin Matandiko na Pamela Chilongola, Mwananchi
Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar
es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema, amemsamehe Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye hivi karibuni
alimtolea maneno makali kutokana na kutofautiana naye juu ya msimamo wa
viongozi wa Kikristo kuhusu Katiba Inayopendekezwa.