Pages

Pages

Pages

Sunday 29 March 2015

MECHI YA URUSI, MONTENEGRO YAVUNJIKA

Wachezaji wa Montenegro
Mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Ulaya kati ya Urusi na Montenegro ilisitishwa baada ya wachezaji kutoka timu zote kupigana uwanjani.

Awali mechi hiyo ilikuwa imesitishwa kwa dakika 30 baada ya mlinda mlango wa Urusi kugongwa na kifaa na kisha kupelekwa hospitalini.
Wakati Urusi ilipopoteza penalti katika kipindi cha pili wachezaji na maafisa kutoka pande zote walianza kupigana.
Kisha mchezaji mwingine wa Urusi aligongwa wakati vifaa zaidi viliporushwa uwanjani hatua iliyomfanya refa kusimamisha mechi hiyo.
Hakuna timu iliyokuwa imefunga bao wakati huo na haijulikani hatua ambayo itachukuliwa na Shirikisho la Soka barani Ulaya.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment