Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 17 December 2014

WAZIRI GHASIA ATIMUA WAKURUGENZI WALIOBORONGA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Waziri wa Nchi Ofisi ya  Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia

Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.


Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda, waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na wa Manispaa ya Sumbawanga.

Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine watatu wakipewa onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.


CREDIT: JAMIIFORUMS

No comments:

Post a Comment