Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 17 December 2014

MEMBE AZINDUA SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Displaying 1.JPG
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu ambaye ndiye kiongozi wa Timu ya Mabalozi wa Tanzania walioanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza mlima na kuvutia wageni wengi zaidi nchini.

Displaying 7.JPG
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajab pamoja na timu ya mabalozi anayoiongoza kupanda Mlima Kilimanjaro akinyanyua juu bendera ya taifa pamoja na kushangilia ikiwa ni ishara ya kuuthamini Mlima Kilimanjaro ambo ni chachu muhimu ya utalii nchini.
Displaying 6.JPG
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa akitoa maelezo ya Mlima Kilimanjaro kwa Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania.
Displaying 5.JPG
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru akitoa neno la ukaribisho kwa Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa.
Displaying 4.JPG
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi muda mfupi kabla ya kuzindua safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza ili kuvutia watalii wengi nchini.
Displaying 3.JPG
Baadhi ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa kabla ya uzinduzi rasmi wa zoezi lao la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza ili uweze kuvutia wageni wengi zaidi nchini.
Displaying 2.JPG
Mabalozi wakiwa tayari kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika lango la Marangu. Kutoka kushoto ni Dk. Batilda Burian; Daniel Njoolay; Aziz Mlima; Joseph Sokoine na Ramadhani Mwinyi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali ulimwenguni kuhakikisha kuwa wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza diplomasia ya uchumi.

Waziri Membe aliyasema hayo wakati akizindua zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro linalofanywa na mabalozi mbalimbali wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi kwa lengo la kuutangaza Mlima Kilimanjaro ili uweze kuvutia watalii wengi zaidi.
“Bado idadi ya watalii wanaofika nchini kupanda mlima hairidhishi na jitihada kubwa zinahitajika kufanywa na mabalozi kuhakikisha kuwa wanautangaza vema mlima kwa kuwa ni hazina ya pekee tuliyonayo inayopaswa kuwa kitega uchumi kizuri kwa uchumi wan chi yetu” alisema Membe.
Jumla ya mabalozi 14 wanashiriki zoezi hili ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuutangaza Mlima Kilimanjaro. Mabalozi hao ni pamoja na Adadi Rajabu (Zimbabwe); Ramadhani Mwinyi (Umoja wa Mataifa); John Kijazi (India); Batilda Burian (Kenya); Shamim Nyanduga (Msumbiji); Grace Mujuma (Zambia); na Patrick Tsere (Malawi).

Wengine ni pamoja na Mbarouk Mbarouk (Saudi Arabia); Joseph Sokoine (Mkurugenzi Bara la Amerika); Ladislaus Komba (Uganda); Azizi Mlima (Malaysia); Radhia Msuya (Afrika Kusini); Daniel Ole Njoolay (Nigeria) na Charles Sanga (Balozi mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii).

No comments:

Post a Comment