Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 12 December 2014

JK ATEUA WAKUU TAASISI ZA SERIKALI NA MAHAKAMA


RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Bi. Katarina Revocati kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa na Bw. Rugalema Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama Kuu, kuanzia Desemba 5 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ilisema awali Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara.

Alisema Bw. Kahyoza kabla ya uteuzi huo, alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi, Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na Mashauri.

Balozi Sefue aliongeza kuwa, Rais Kikwete pia amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia Desemba 4 mwaka huu ambapo awali alikuwa Naibu Mkuu TEWW.

Pia Rais Kikwete amemteua Profesa Dominic Kambarage, kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kipya cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia Desemba 5 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kambarage alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, mkoani Morogoro.

Alisema kuwa, kutokana na kuanzishwa kwa Chuo hicho kingine cha Umma, Rais Kikwete pia amemteua Profesa Lesakit Mellau kuwa Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho upande wa Taaluma kuanzia Desemba 5 mwaka huu.

Aliongeza kuwa, kabla ya uteuzi huo, Prof. Mellau alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

Rais Kikwete pia amemteua Profesa Msafiri Jackson kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Utawala) kuanzia Desemba 5 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Jackson alikuwa Mratibu wa Masomo ya Taaluma za Shahada za Juu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemteua Bw.Laurence Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia Novemba 5 mwaka huu ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha, Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (PDB).

Pia Bw. Mafuru alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa muda wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Rais Kikwete pia amemteua Bi. BengĂ­i Issa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuanzia Desemba 4 mwaka huu. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Fedha katika Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).

CREDIT: MAJIRA

No comments:

Post a Comment