Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wa pili kulia) akimkaribisha Balozi
wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) pamoja na maofisa wa ubalozi huo,
ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe na Balozi huyo
walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya
Balozi huyo nchini.
Balozi
wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri
Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na wizara.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa
Marekani nchini, Mark Childress kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini. Balozi Childress alimtembelea
Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA
MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment