Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akipokea msaada wa
vifaa mbalimbali vya kuzima moto pamoja na makoti ya kujikinga na kemikali,
kutoka kwa Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose (kulia). Msaada wa vifaa
hivyo ambavyo tayari vimeingia nchini kwenye kontena maalumu pia kuna kofia
ngumu kwa ajili ya Jeshi la Polisi, pamoja na aina mbalimbali ya mabuti jeshi,
suruali maalumu kwa ajili ya kupambana katika matukio mbalimbali na viatu vya
kiume na kike. Kushoto ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi,
Paulo Chagonja na Kaimu Kamishna Operesheneni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
Christom Manyologa ambao walikabidhiwa vifaa hivyo baada ya kupokelewa na
Waziri Chikawe katika ukumbi wa wizara hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimshukuru Balozi wa
Uingereza nchini, Dianna Melrose kwa msaada wa vifaa mbalimbali vya kuzima moto pamoja na
makoti ya kujikinga na kemikali ambayo vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya
Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kukabiliana na matukio
mbalimbali nchini.
Picha zote na Felix
Mwagara Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment