Waziri mkuu mteule Narendra Modi |
Kiongozi wa upinzani nchini
India, Narendra Modi, atakuwa waziri mkuu mpya katika taifa hilo ambalo lina
historia ndefu ya demokrasia, akishinda uchaguzi muhimu kuwahi kushuhudiwa
katika nchi hiyo kwa miongo mitatu.
Modi na chama chake cha
Hindu Nationalist amekiamngusha chama cha Congress ambacho kimekuwa kikidhibiti
siasa za nchi hiyo kwa muda mrefu .
Modi, ambaye ni
mwanasiasa mzoefu ambaye katika kampeni yake ameahidi kuufufua uchumi wa nchi
hiyo, atakuwa na mamlaka makubwa kutawala katika wakati wa mabadiliko makubwa
katika jamii ya India. Pia amesema kuwa anataka kuimarisha uhusiano wa
kimkakati na Marekani.
Lakini wakosoaji wanahofu
kwamba kuingia madarakani kwa chama chake cha wazalendo cha Wahindu kunaweza
kuhatarisha hali ya wasi wasi wa kimadhehebu na Waislamu wa India wapatao
milioni 138 ambao ni wachache nchini humo.
Congress yaporomoka
Matokeo yalikuwa ni
kipigo kikubwa kwa chama cha Congress, ambacho kinamafungamano makubwa na ukoo
wa kisiasa wa Nehru-Gandhi ambacho kimekuwa katikati ya siasa za India kwa muda
wa historia ya nchi hiyo ya baada ya uhuru.
Serikali , ikiongozwa na
waziri mkuu anayeondoka madarakani Manmohan Singh, imekabiliwa na kashafa za
mara kwa mara za rushwa na uchumi mbovu.
Wakati ushindi wake wa
kishindo ulipoanza kuonekana wazi kuanzia siku ya Ijumaa, Modi alijitokeza
katika kundi la waungaji wake mkono waliokuwa wakishangiria na kujaribu kutoa
matamshi ya maridhiano.
"Nimekuwa nikisema
kila wakati kuwa kuongoza taifa ni wajibu wetu kuwajumuisha kila mtu pamoja
nasi," Modi amesema baada ya uchaguzi mrefu na uliohitaji kazi ngumu.
"Nahitaji ridhaa yenu ili tuweze kuiendesha serikali ambayo inabeba kila
mtu pamoja."
Ni kiongozi anayeleta
mtengano
Pamoja na hayo , Modi
anabaki kuwa mtu anayeleta mtengano katika nchi hiyo yenye wakaazi bilioni 1.2,
kwa kiasi kikubwa kwa sababu, yeye kama waziri kiongozi wa jimbo la Gujarat,
alikuwa mamlakani mwaka 2002 wakati ghasia za kikabila katika jimbo hilo ziliposababisha
vifo vya zaidi ya watu 1,000, wengi wao Waislamu.
Modi alishutumiwa kwa
kutofanya vya kutosha kuzuwia ghasia hizo, licha ya kuwa anakana kosa lolote na
hajafunguliwa mashtaka kwa uhalifu. Alikataliwa visa kuingia nchini Marekani
mwaka 2005 kwa madai ya kuhusika katika ghasia hizo, licha ya kuwa kama waziri
mkuu atakuwa na hakika ya kupata visa kuingia nchini Marekani.
Obama ampongeza Modi
Jana Ijumaa(16.05.2014)
rais Barack Obama wa Mareakani amempigia simu Modi na kumpongeza kwa ushindi na
kumwalika "kutembelea Washington katika muda ambao utakubalika na pande
zote ili kuimarisha uhusiano wa mataifa yetu," Ikulu ya Marekani imesema
katika taarifa.
Utawala wa Marekani
ulikuwa unaangalia kunyanyuka kwa Modi kwa karibu, na mwezi Februari, kwa mara
ya kwanza katika muda wa uongozi wa karne moja kama afisa wa ngazi ya juu wa
jimbo la Gujarat, balozi wa Marekani alikutana nae.
Nchini
India , suala sasa ni iwapo Modi anaweza kweli kuwa kiongozi anayetenganisha
dini na serikali katika nchi hiyo ambayo ina waumini wa imani nyingi.
Chama
cha Congress kilijaribu kuibua hali ya ghasia za mwaka 2002, katika kampeni,
lakini kasi ya Modi na kutoangalia sana udhaifu wa uchumi, umemfikisha katika
ushindi.
CHANZO, DW.DE.COM/SWAHILI
|
No comments:
Post a Comment