TAIFA KWANZA!

Pages

  • Home
  • KILIMO ENDELEVU
  • KILIMO HAI
  • CONTACTS US

Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 17 May 2014

TAARIFA YA UFUATILIAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE


WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

TAARIFA YA UFUATILIAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE

1.    UTANGULIZI
Mnamo tarehe 27 Januari 2014, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya dengue katika Kliniki ya ‘International School of Tanganyika’ iliyopo Manispaa ya Kinondoni katika jiji la Dar es Salaam. Taarifa hiyo ya awali ilionyesha kuwepo kwa jumla ya wagonjwa 6 katika kituo hicho bila vifo.

Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es salaam ambapo idadi ya watu 40 walithibitika kuwa na
ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai 2013,  wagonjwa 172 walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.
2.    UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes. Dalili za ugonjwa huu ni homa ya ghafla,mwili kuchoka,  kuumwa na viungo, kuvimba tezi na kupatwa na harara. Uwepo wa homa, kuumwa kichwa  maumivu ya viungo na uchovu ndio dalili kuu  za ugonjwa huu. Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati  siku ya 3 na 14 tangu mtu alipoambukiwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwingine  dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria. Kuna aina 3 tofauti za namna ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi hivi;

        i.     Homa ya dengue (Dengue Febrile Illness): Aina hii huambatana  na dalili kuu tatu za homa kali ya ghafla, kuumwa kichwa na maumivu ya viungo au uchovu. Asilimia kubwa ya watu hapa nchini waliothirika wamekuwa na aina hii ya dalili.

       ii.     Dengue ya damu (Dengue Haemorrhagic Fever): Aina hii ya  homa ya dengue huambatana na dalili za mgonjwa kutokwa na damu kwenye fizi au puani, vile vile kutokwa na damu chini ya ngozi.  Iwapo mgonjwa huyu ataumia sehemu yoyote ni rahisi kwake kupoteza damu nyingi kupitia kwenye michubuko.

     iii.     Dengue ya kupoteza fahamu (Dengue Shock syndrome): Aina hii ya homa ya  dengue huambatana na mgonjwa kupoteza damu nyingi ambayo hupelekea mgonjwa  kupoteza fahamu.

Aina ya pili na ya tatu ni aina zenye dalili mbaya ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa na hatimaye kusababisha kifo. Kwa Tanzania, hadi sasa ni aina ya kwanza ya Homa ya Dengue imeripotiwa.

Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu  baada ya kuumwa na mbu aina ya “Aedes”. Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu.

Ugonjwa huu hauenezwi moja kwa moja kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine bali kwa kupitia  mbu aliyeambukizwa na virusi vya homa ya dengue anapomuuma binadamu. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka. Hakuna tiba maalum ya kutibu virusi vya denge wala chanjo  bali mgonjwa anatibiwa kutokana na  dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue:

o   Kuangamiza mazalio ya mbu 
ü  Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama  au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi  vya mbu kwenye madimbwi hayo 
ü  Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile, vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
ü  Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
ü  Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo yaharuhusu maji kutuma
ü  Funika mashimo ya maji taka  kwa mfuniko imara
ü  Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama

o   Kujikinga na kuumwa na mbu
ü  Tumia dawa za kufukuza mbu “mosquito repellants”
ü  Vaa nguo ndefu
ü  Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (hasa kwa wale wanalala majira ya mchana)
ü  Weka wavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi

2. HALI HALISI YA SASA YA UGONJWA NCHINI

11.1  Idadi ya Wagonjwa:
Kuanzia tarehe 27 Januari hadi tarehe 6 April 2014, jumla ya wagonjwa 399 (Kinondoni – 322, Ilala – 61 na Temeke – 16) wamethibitishwa  kuwa na ugonjwa homa ya dengue.  kati yao, wagonjwa wawili (2) wamepoteza maisha;

(i)  Mwanamke, umri miaka 22, aliyefariki katika Hospitali ya Mwananyamala tarehe 14.3.2014.

(ii) Mwanamke, umri miaka 37, muuguzi, aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Temeke ambaye alifia hospitali ya MNH

11.2  Maeneo yaliyoathirika

Ugonjwa huu umeripotiwa katika kila eneo la Dar es salaam lakini Kata zilizoathirika zaidi kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi ni kama zifuatatazo;

KATA
IDADI
Msasani
93
Masaki
68
Magomeni
54
Kinondoni A/B/Manyanya
29
Mikocheni
21
Buguruni
20
Tandale
15
Sinza/Kijitonyama
13

11.3  Dalili za kuu zilizojitokeza
Wagonjwa wote 399 waliothibitishwa kuwa na ugonjwa walikuwa na  na homa kali..  Aidha 82% ya wagonjwa walionyesha pia dalli ya kuumwa kichwa. Dalili nyingine ni zilizojitokeza ni pamoja na kutapika, maumivu wakati wa kutoa haja ndogo,  na kuumwa tumbo.

11.4  Jinsia na Umri
Kati ya Wagonjwa 376, 214 (54%) walikuwa wanaume na 185(46%) walikuwa ni wanawake. Idadi kubwa ya wagonjwa waliothibitika kuwa na ugonjwa huu wako katika Umri zaidi ya miaka 16 yaani  asilimia 92. Aidha watoto chini ya umri wa miaka 5 walikuwa ni asilimia 2 tu.

1.1   Mwenendo wa Ugonjwa
Mlipuko huu wa tatu wa dengue hapa nchini ulianza tarehe 2 Januari 2014. Ongezeko kubwa la wagonjwa limejitokeza katika mwezi wa tatu (3) mwishoni na kushika kasi mwezi wa Aprili, 2014 ambapo wagonjwa wengi wameongezeka.

Jedwali No 1: Mwenendo wa Ugonjwa wa Dengue kuanzia utokee,2  Januari 2014- 6 May 2014 (N=399)
2.    HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA WIZARA
2.1  Hatua za Muda mfupi
ü  WAUJ imetoa  tamko la Serikali kwa wananchi kwa nyakati tofauti kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza lilitolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014.  Aidha, uelimishaji kwa wananchi unaendelea kupitia Radio, TV na magazeti. Aidha matumizi ya Vipaza sauti katika ngazi za chini utaanza na kusimamiwa na Halmashauri za Wilaya mkoani Dar es salaam.  

ü  Kuendelea kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia inajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Ukweli Kuhusu Ugonjwa“(Fact sheet)  na mwongozo wa uchukuaji wa sampuli na matibabu. 

ü  Kuendelea kutoa elimu kwa Watumishi wa afya madaktari pamoja na wanaofanya maabara kuhusu namna ya kutambua ugonjwa huu. Aidha watumishi wa hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke wamekwisha kupewa mafunzo haya na bado yanaendelea  kutolewa kupitia mikutano ya kila asubuhi ya kiltaaluma (Clinical meetings). Halmashauri zinaendelea pia kuyatoa mafunzo haya katika ngazi za chini.

ü  Kufuatilia kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa Mikoa na Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu.

ü  Kuanzishwa kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika Hospitali za Manispaa za jiji la Dar es Salaam (Mwananyamala, Amana na Temeke Hospitali), aidha, Kituo cha ‘ International School of Tanganyika – IST’ kilichopo Manispaa ya Kinondoni pia kinaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu pamoja na Kituo cha Hospital ya Muhimbili.

ü  Kuimarisha uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya Taifa (NHLQATC) ambapo mpaka sasa kumethibitishwa kuwepo kwa aina 2 za virusi hivi yaani DENV2 na DENV3. Vile vile Wizara imepeleka kiasi kidogo cha vipimo vya awali yaani “Dengue Rapid Test Kits” kwa baadhi ya vituo vya Dar es salaam kuimarisha utambuzi na vituo hivo ni pamoja na Muhimbili, Amana hospital, Mwananyamala hospitali, Temeke Hospital, na IST kliniki.

ü  Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mipakani kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa (saveilensi) ya IDSR . Aidha,  Wizara imetoa maelekezo kwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya kutoa taarifa za wagonjwa wa Dengue Fever kupitia taarifa za kila wiki (Infectious disease week ending).

ü  Kutoa miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani kuhusu kutokuwepo kwa aina yoyote ya vikwazo vitakavyowekwa kwa ajili kwa wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha kuwa iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.

ü  Kudhibiti mbu kwa kupulizia dawa ( Fogging) katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika katika mkoa wa Dar es salaam. Aidha mpango wa WAUJ ni kufikia maeneo mengi zaidi pamoja na kufanya kuweka dawa ya kuua viliwi luwi (Larviciding)” kwa viluwiluwi.

ü  Kupeleka taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama mwongozo wa Kimataifa uvyaoelekeza.

ü  Kupitia Timu ya Taifa ya Maafa, Wizara imeandaa  mpango kazi na mkakati wa muda mfupi wa namna ambavyo ugonjwa huu utadhibitiwa ukishirikisha wadau mbalimbali. Kimabatanisho namba 1 kinafafanua kazi zilizoaninishwa.

3.2 Hatua za muda mrefu

ü  WAUJ imeandaa Mpango Mkakati (2014 – 2018) wa kukabiliana na magonjwa ya ‘Viral Haemerrhagic Fevers’ ikihusisha na ugonjwa wa homa ya dengue.

ü  Halmashauri za mkoa kutengeneza “strategic plan” ya kwao kwa kuangalia “prototype plan” ya WAUJ

4.    Changamoto
4.1  Kutokuwepo na vitendanishi vya kutosha kuanisha ugonjwa huu kwa ngazi za chini (Rapid Diagnostic kits). Hii inapelekea ufuatiliaji wa ugonjwa huu kuwa mgumu kwa watumishi wa vituo vya afya na kulazimu sampuli zipelekwe Maabara kuu ya Taifa -- NHLQATC.

4.2  Kutokuwepo na mpango mkakati shirikishi wa pamoja na wadau mbalimbali wa namna ya kukabiliana na ugonjwa huu. Aidha Wizara imeitisha mkutano wa pamoja na wadau ili kuweza kushirikiana nao. Mkutano huu umefanyika 7.5.2014 ambao umeainisha hatua za kuchukuliwa.

4.3  Upungufu wa wataalum waliobobea katika kukabiliana na wadudu wadhurifu “Entomologists” katika ngazi ya mbalimbali. Na hii inapelekea uratibu wa kazi za “vector ” kutoratibiwa katika kiwango  stahiki.

4.4  Kutokuwepo na fedha za kutekeleza mikakati mbalimbali ya “Integrated Vector control activities” pamoja  na kukabiliana na milipuko kwa ujumla kutoka ngazi ya Taifa mpaka chini.

4.5  Jamii kutokukuelewa kuhusu ugonjwa huu na hii ni kwa sababu ugonjwa huu bado ni mpya nchini Tanzania. Kupitia mpango mkakati unaoandaliwa na Wizara, ushirikishwaji wa wadau wengine zaidi ya wa afya utaanishwa ili kuweza kuandaa vielemishi na kutafuta njia nyingine za kufikisha ujumbe.

Kiambatanisho namba 1,
MAAZIMIO YA KIKAO CHA TIMU YA TAIFA YA MAAFA KUHUSUIANA NA DENGUE FEVER

TAREHE 7.5.2014
Kazi
Shughuli
Mhusika
Muda wa Utekelezaji
Uratibu wa shughuli za Dengue Kitaifa
Kuwasilisha mpango kazi ulioandaliwa kwa ngazi za juu ili pia uweze kuwasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu
WAUJ: Epidemiolojia
Mara moja
Uratibu wa shughuli za Dengue mkoani Dar es salaam
Kuandaa mpango mkakati wa namna ya kukabiliana na Dengue kwa kutumia prototype plan ya mpango mkakati wa Kitaifa
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Tarehe 12.5.2014
Udhibiti wa Mbu na viluwiluwi
Kuua mazalio ya mbu yaani viluwili (Larvidicing) kwa kutumia bio-larvicide –ambao iko kwa kiasi iliyokuwa inatumika katika mradi wa Bio larvicide kati ya Cuba na WAUJ kupitia NMCP. Aidha kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
Kuendelea na kufanya fogging (kuua mbu wapevu) wenye tayari vimelea kutumia viautilifu vya  kuua mbu katika maeneo yaliyotoka idadi ya wagonjwa wengi. Aidha kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja (Angalizo: utategemea pia hali ya hewa na mvua)
Usafi wa mazingira: Maafisa Afya wote wa Halmashauri  watahusika katika kusimamia na kuhamasisha usafi wa mazingira kwa kutumia sheria ndogo ndogo ilizojiwekea ikiwemo na kutoa faini
WAUJ: Kitengo cha Usafi wa Mazingira
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja
Maafisa Afya  ikiwemo wa kata wataelemisha  wananchi namna ya kudhibiti ugonjwa kwa  vipaza sauti, uongozi wa mitaa, kugawa vielemishi. Na vilevile kuendelea kutumia vyombo vya habari na TV
WAUJ: Kitengo cha Usafi cha mazingira na Elimu ya Afya
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Elimu kwa watumishi wa Afya
Kutoa elimu kupitia clinical meetings katika hospitali zote za wilaya na pia kupitia APHTA
WAUJ: Epidemiolojia
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja
Kuimarisha utambuzi wa ugonjwa
WAUJ kuwasiliana na MSD kuhusu upatikanaji wa “Dengue Rapid Kits” ili Halmashauri ziweze kufuata utaratibu wa manunuzi
Halmashauri na pia MNH kupanga katika mipango yao fedha za kununua kits hizi
Kwa kipindi hiki ambapo “kits” zinaonekana kupungua katika maeneo tajwa yaani MNH, na Hospital za Wilaya mkoani Dar es salaam, NHLQATC itatumika kupima vipimo hivi ili kuwepo na mwenendelezo wa “Sentinel Surveillance”
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja
Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa
Kutengeneza protocol ya Surveillance pamoja na alogarithm ya matibabu
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
10.5.2014
Kuweka “messages” katika Point of Entry
WAUJ: Kitengo cha Afya ya Mazingira
Mara moja
Ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huu
WAUJ kuandika barua kwa RAS Dar es saalam kuanisha maeneo ya utekelezaji ambao yako chini ya mamlaka yake
WAUJ kuandika barua ya kuomba  zaidi msaada wa “Dengue Rapid Kits” WHO, CDC na USAID
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
Mara moja
UNICEF kusaidia na IEC materials yaani Posters na leaflets ambazo tayari zimeshatengenezwa
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
Mara moja maana tayari kuna mawasiliano
WHO kusaidia katika uelimishaji kwa kupitia kifungu cha fedha za “World Health Day” iliyolenga masuala ya “vector”
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
Utekelezaji unategemea barua kuandikwa kutoka WAUJ kwenda WHO

Imeandaliwa na:
Kitengo cha Epidemiolojia na Ufuatiliaji wa Magonjwa

May, 2014
Posted by http://taifakwanza5.blogspot.com/ at Saturday, May 17, 2014
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

SOMA WAJIBIKA AGOSTI 17-23, 2015

SOMA WAJIBIKA AGOSTI 17-23, 2015

ANGALIA MADA MBALIMBALI

  • BIASHARA (35)
  • BIASHARA NA UCHUMI (341)
  • BURUDANI (299)
  • ENZI HIZO ZAMANI (30)
  • JAMII (1669)
  • KIMATAIFA (383)
  • KITAIFA (990)
  • MATOKEO YA AJABU (13)
  • MICHEZO (619)
  • SAIKOLOJIA (13)
  • SAYANSI NA MAZINGIRA (47)
  • SIASA (628)
  • TUNGO MARIDHAWA (5)
  • UCHUNGUZI (67)
  • UTALII (138)
  • VUNJA MBAVU (5)

Contributors

  • Unknown
  • Unknown
  • Unknown
  • http://taifakwanza5.blogspot.com/

WANAOTEMBELEA BLOG HII

TANGAZA NASI

WASILIANA NASI

Simu: + 255 656 331 974/ + 255 787 426 161
Barua-Pepe: brotherdanny5@gmail.com

BLOG MARAFIKI ZETU

SALUTI5
JIACHIE
MJENGWABLOG
GLOBALPUBLISHERS
BIN ZUBEIRY
MICHUZI BLOG
MTANDA BLOG
UDAKU SPECIALLY
THE BLACK SAMURAI
SUPERD BOXING COACH

addyourblog

Blog Promotion Top Blogs
Promote Your Blog
Free Blog Directory
Blogs Tools Scented Candles

TaifaKwanza!

Your Website Title

TAFUTA HAPA

Pages

  • Home

Networkedblogs

Follow this blog

Pages

  • Home

Google An

Share

FOLLOW US ON

Instagram

Translate

LIVE - Kwanza Jamii radio

Follow this blog

BLOG UP

Search This Blog

blogssumary

www.chatguest.com
HyperSmash

Blog Promotion Top Blogs
Promote Your Blog
Free Blog Directory
Blogs Tools Scented Candles

Popular Posts

  • BARUA KUTOKA KWA MUME WA FLORA MBASHA KWENDA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA
    "Mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu M...
  • HUYU NDIYE BOSI WA HOME SHOPPING CENTRE AMBAYE AMEKUWA BALOZI WETU CHINA!
    Huyu ndiye Salaah, bosi wa Home Shopping Centre ambaye serikali yetu tukufu imemteua kuwa Balozi Mdogo huko China.
  • UTAJIRI WA RIDHIWANI KIKWETE...
    Ndugu zangu, mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu Familia Nambari Moja Tanzania, hasa 'festi boni' wa Rais Kikwete, Ridhiwani, kwamba ...
  • NDOA YA NASSARI, HALIMA MDEE YAOTA MBAWA, JAMAA ANAOA KESHO!
    Joshua Nassari na Halima Mdee, mwaka 2012 Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Meru UWEZEKANO wa kuwepo kwa ndoa baina ya mbu...
  • HUYU NDIYE SUPER MOGUL DAVIS MOSHA MTANZANIA WA KWANZA KUMILIKI GARI LA AJABU HAPA BONGO ONA HAPA MWENYEWE LIVE!!
    Gari la aina ya Lamboghirn gharama yake kwa hela za Tanzania ni Shillingi Billioni Moja na Nusu (1,500,000,000). Davis anakuwa Mtanza...
  • MKUYU: MALKIA WA MITI YOTE
    *Baadhi wanauita mti mtakatifu, wengine wanasema wa mashetani Na DANIEL MBEGA TANGU utotoni tulizowea kuambiwa kwamba mti...
  • MECHI YA 77 SIMBA NA YANGA LIGI KUU TANGU 1965
    Picha kwa hisani ya sw-ke.facebook.com Na Daniel Mbega “KITIMTIMU, mtakiona leo, nyumba ya shetani mwendawazimu kaingiaje!” Naam,...
  • ETI PENZI LA MAMA MKWE TAMU KULIKO LA MKEWE! DUNIA KWELI INA MAMBO, SIKIA KISA HIKI
    Kuishi kwingi ni kuona mengi. Unaweza kusema dunia imekwisha. La Hasha! Wanadamu ndio wamebadilika, wamekuwa kama wanyama. Hata wanyama we...
  • TOA MAONI, BORESHA MUSWAADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI
    Na Mwandishi Wetu Mwanadamu katika maumbile yake amejengeka katika falsafa ya kufafuta ukweli na kuupambanua na taarifa zinazokinzana na ...
  • KUPOTEZA BIKIRA
    Picha ya mtandaoni VIJANA wenzangu, natumaini mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku katika ujenzi wa taifa na j...

Followers

Blog Archive

  • ►  2022 (1)
    • ►  February (1)
  • ►  2020 (3)
    • ►  August (2)
    • ►  February (1)
  • ►  2019 (8)
    • ►  April (2)
    • ►  March (6)
  • ►  2017 (152)
    • ►  January (152)
  • ►  2016 (2321)
    • ►  December (183)
    • ►  November (191)
    • ►  October (111)
    • ►  September (271)
    • ►  August (227)
    • ►  July (135)
    • ►  June (118)
    • ►  May (187)
    • ►  April (158)
    • ►  March (285)
    • ►  February (332)
    • ►  January (123)
  • ►  2015 (3346)
    • ►  December (232)
    • ►  November (89)
    • ►  October (223)
    • ►  September (336)
    • ►  August (504)
    • ►  July (341)
    • ►  June (350)
    • ►  May (452)
    • ►  April (354)
    • ►  March (310)
    • ►  January (155)
  • ▼  2014 (3967)
    • ►  December (285)
    • ►  November (505)
    • ►  October (515)
    • ►  September (423)
    • ►  August (327)
    • ►  July (279)
    • ►  June (463)
    • ▼  May (372)
      • BABA MZAZI WA SERGIO AGUERO ADAI MWANAYE ANAPENDA ...
      • MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA WIKI YA MAZINGIR...
      • SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJEN...
      • ACADEMIE TCHITE YAISHIKISHA ADABU AL-MERREIKH, MBE...
      • MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AFARIKI DUNIA BAADA ...
      • DIAMOND NDANI WA WASHINGTON DC, APIGA PICHA NA MAS...
      • KILIMO NI UTI WA MGONGO, LAZIMA MFUMO MZIMA UBORES...
      • WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA NA WAZIRI WA NISHAT...
      • WAWILI KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA KUPITIA SHINDANO ...
      • KORONGO WA KAMPALA KAZI NZITO NA MADAGASCAR , TAIF...
      • TANZIA: MUONGOZAJI WA FILAMU, GEORGE TYSON AMEFARIKI!
      • WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UTURUKI AKUTANA NA RAIS ...
      • DA' JOY 'CHALI' MALAWI, PETER MUTHARIKA NDIYE RAIS...
      • HEMEDI MANETI ATIMIZA MIAKA 24 KABURINI!
      • MWANAMITINDO RODNEY AFARIKI DUNIA, KUZIKWA JUMAMOS...
      • MWANZA KUMEKUCHA WASANII WAWASILI KWENYE KILI MUSI...
      • SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAANZA RASMI JA...
      • NORWAY NA ZANZIBAR ZATILIANA SAINI UNENGWAJI WA WO...
      • PRESIDENT KIKWETE, CANADIAN PRIME MINISTER STEPHEN...
      • PRESIDENT KIKWETE MEETS PRESIDENT OF THE WORLD BAN...
      • ARSENE WENGER HAONDOKI ARSENAL HADI 2017
      • KAMBI RASMI YA UPINZANI YASUSIA BAJETI YA NISHATI
      • PRESIDENT KIKWETE MEETS MELINDA GATES AND CANADIAN...
      • TAARIFA YA LAPF KUHUSU KUMKOPESHA FEDHA MBOWE KUWA...
      • QUARTER FINAL FIXTURE FOR CECAFA NILE BASIN CUP
      • SHUKRANI: PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU
      • DK. REGINALD MENGI AJIBU TUHUMA
      • NI ROBO FAINALI YA NILE BASIN LEO NA KESHO
      • WHITE HOUSE YASHUTUMU SILAHA ZA URUSI
      • FRANK LEONARD APATA TUZO YA TANAPA
      • MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA MKE WA KA...
      • MAGEREZA NA GEPF WATILIANA MKATABA WA UWEKEZAJI
      • SAMATA, ULIMWENGU KUIONGEZEA NGUVU STARS
      • SIX TELECOMS, TATA COMMUNICATIONS WAZINDUA MTANDAO...
      • MAKAMU WA RAIS DKT. BILA AFUNGUA MKUTANO WA TATU W...
      • SERIKALI KUENDELEA KUTHAMINI NA KUSIMAMIA MAENDELE...
      • MILIONI MOJA NA NUSU ZACHANGWA KUNUSURU HOTELI YA ...
      • MIGOGORO YA ARDHI YAWA KERO KUBWA MKOANI MANYARA, ...
      • BALOZI MDOGO MISRI AMUAAGA RAIS DKT SHEIN
      • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA MFUKO WA PENS...
      • MTOTO SHIGELA ALIYEZALIWA NA VVU AAGA DUNIA JIJINI...
      • “WE WILL NOT HESITATE TO CONTRIBUTE MORE PEACEKEEP...
      • ABDEL-FATTAH AL-SISI NDIYE RAIS MPYA WA MISRI
      • AFRICA’S LONGEST-KNOWN TERRESTRIAL WILDLIFE MIGRAT...
      • "WE WILL NOT HESITATE TO CONTRIBUTE MORE PEACEKEEP...
      • WABAKWA KISHA KUNYONGWA
      • RAIS GOODLUCK ATANGAZA VITA KALI NA BOKO HARAM
      • WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUFANYA UTAFITI
      • KIWANDA CHA NGOZI ARUSHA BADO CHAPIGWA KUFULI KWA ...
      • SERIKALI YAOMBWA KUWAPATIA BIMA WATOTO
      • MWANAFUNZI MLEMAVU MIKONO YOTE MIWILI AOMBA MSAADA...
      • BUNGENI LEO
      • SERENA, VENUS NJE FRENCH OPEN
      • MSIBA MKUBWA MAN UNITED
      • MKUU WA JESHI SOMALIA ANUSURIKA KUUAWA NA AL SHABAAB
      • MBEYA CITY FC WATINGA ROBO FAINALI YA CECAFA NILE ...
      • MUME AMSHTAKI MKEWE KWA KUMNYIMA UNYUMBA
      • UN YALAANI KUUAWA KWA MWANAMKE PAKISTAN
      • UCHUMI WA AFRIKA UNAPIGWA MSASA LEO MSUMBIJI
      • MATOKEO YA UCHAGUZI MALAWI SASA NI KESHO IJUMAA
      • HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZAR...
      • HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZAR...
      • HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZAR...
      • HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZAR...
      • HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZAR...
      • HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZAR...
      • MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL A AFUNGUA MKUTANO MKUU W...
      • KINANA AUNGURUMA MBULU,AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
      • WAZIRI MKUU MHE. PINDA NA MATUKIO KATIKA PICHA BUN...
      • JUMA MWAMBUSI WA MBEYA CITY ATWAA TUZO YA KOCHA BO...
      • ZOEZI LA UKAGUZI WA STEMPU KWENYE BIDHAA ZA FILAMU...
      • OAK YAJADILI HAKI ZA WATOTO
      • WANACHAMA WA SIMBA WAANDAMANA NA KUFUNGA NJIA ZA M...
      • MO ATAKA MADHEBEBU YA DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKAL...
      • AZAKI ZAANDAA MDAHALO WA KATIBA
      • TAARIFA YA WIZARA KUHUSU ZAWADI ZA WANAFUNZI WALIO...
      • TAARIFA ZA WALIOWEKEANA PINGAMIZI SIMBA SC
      • HAWA NDIO WANAODAIWA KUUNDA KUNDI LA 'MBWA MWITU'
      • POCHETTINO KUINOA TOTTENHAM KWA MIAKA MITANO
      • MWANAMKE ALIYEHUKUMIWA KIFO SUDAN AJIFUNGUA AKIWA ...
      • MEMBE: M23 WALITOKA RWANDA
      • AL SHABAAB WAKIRI KUSHAMBULIA DJIOBOUTI
      • OBAMA ASEMA WANAJESHI 10,000 KUBAKI AFGHANISTAN
      • BARAZA LA MADIWANI ARUSHA LATOA SIKU 30 KUKAMATWA ...
      • MEYA ARUSHA ALIA NA WATOTO WANAOPANGIWA MBALI NA S...
      • RODGERS AMWAGA WINO ANFIELD
      • CAMEROON YASHINDA LICHA YA MAJERAHA
      • PAPA FRANCIS ASHUTUMU MAPADRE WALAWITI KANISANI
      • WAPIGANAJI 30 WAUAWA UKRAINE
      • HATIMAYE MALAYSIA YATOA DATA KUHUSU NDEGE YA MH370...
      • JESHI NIGERIA: 'TUNAJUA WALIKO WASICHANA WALIOTEKE...
      • KATIBU MKUU WA CCM AMALIZA ZIARA SINGIDA, KESHO ZA...
      • DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA WAHADHIRI CHUO KIKUU CAIRO
      • WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WAFANYA ZIARA NA WAANDI...
      • WASHINDI WA BIMA YA JUBILEE TANZANIA WAKABIDHIWA Z...
      • HILI NDILO KANISA LA WALA NYASI, JAMANI DUNIA INAK...
      • UCHAGUZI WA MALAWI WAGEUKA 'SARAKASI'
      • WANAWAKE TASA SASA KUSHIKA MIMBA KUPITIA SAYANSI
      • NIGERIA YAICHAPA AMAVUBI KIGALI 4-1
      • TP MAZEMBE YAICHAPA AS VITA 1-0
    • ►  April (265)
    • ►  March (208)
    • ►  February (113)
    • ►  January (212)
  • ►  2013 (308)
    • ►  December (109)
    • ►  November (77)
    • ►  October (122)
Theme images by Raycat. Powered by Blogger.