Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 17 May 2014

DUNIA IMEKWISHA, KANISA LINAPOWALAZIMISHA WAUMINI WALE MAJANI KAMA MBUZI

Ndugu zangu,
Kadiri siku zinavyosonga mbele, tunashuhudia mauzauza mengi duniani hasa katika masuala ya imani ya dini.
Mfumuko wa madhehebu mengi mengi ya dini umefikia mahali sasa watu wanaibuka na 'ndoto' ambazo zimewafanya wawageuze binadamu wenzao kama hayawani.
Ilielezwa hivi karibuni kwamba kuna kanisa ambalo limeanzia nchini Afrika Kusini, ambapo kiongozi wake anawahubiria waumini wake wale nyasi kama mbuzi, eti ndiyo imani halisi.
Kanisa hili tumeambiwa tayari liko Tanzania, tena jijini Dar es Salaam, ambako waumini wa kanisa hilo wameonekana wakila nyasi kama mbuzi na kutambaa kama nyoka.
Haya ni maajabu makubwa katika karne hii ambayo kwa uhakika yanadhihirisha ujio wa siku za mwisho, ambazo hatujui zitafikia kilele lini.
Huko nyuma tuliwahi kushuhudia Bwana Kibwetere kule Uganda ambaye aliwafungia waumini wake wote kanisa na kuwateketeza kwa moto. Eti ndiyo imani halisi!
Tulishuhudia pia wale ndugu zetu ambao walitaka kwenda Ulaya bila kuwa na paspoti wala tiketi. Wakasema tiketi na paspoti zao ni Biblia. Walirudia Uwanja wa Ndege pale Dar es Salaam.
Walipozuiwa wakaamua kukimbilia msituni wakifunga na kuomba kwamba Yesu angerudi katika tarehe waliyoitaja. Hakuja!
Ndugu zangu,
Sina nia mbaya ya kuwakosoa wenye imani hizi, lakini najaribu tu kuwakumbusha kuhusu maajabu haya yanayoendelea kutokea kila siku ambayo kwa kweli kama hatukuwa makini tunaweza kujikuta tunaacha imai yetu ya kwanza na kupotea kabisa.
Chunga sana ulicho nacho, asije muovu akakupotosha!
Mungu awabariki sana.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa, Tanzania

No comments:

Post a Comment