Wajumbe
wa bunge la kutoka vyama vya upinzani vya CUF. Chadema, NCCR , Dp, NRA,
NLD na Udp ambao wanaunda umoja wao unaojulikana Kama Ukawa wamesusia
bunge na kuondoka bungeni kwa kushindwa kuvumilia hoja zinazotolewa na
wapinzani wao wakuu kutoka chama tawala.
Mwenyekiti
wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ameliambia bunge la katiba takriban saa
10.30 leo jioni kuwa wamechoka kusikiliza hoja za wajumbe wanaotaka
muundo wa serikali mbili kinyume na mapendekezo yaliyotolewa na rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.
Mara
baada ya kumaliza kuzungumza na kuwaaga wajumbe wa bunge Hilo kwa niaba
ya wajumbe wa Ukawa prof. Lipumba aliwaongoza wajumbe wenzake wa Ukawa
kutoka nje ya bunge.
Hata
hivyo Wajumbe hao walioaga bunge kupitia prof Lipumba walitoka bungeni
kuelekea katika ukumbi wa msekwa kufanya kikao cha ukawa huku Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba mh. Samia Suluhu Hassan ameendelea
kuliongoza bunge Hilo kwa wajumbe kuendelea kuchangia.
Wengi wa wajumbe kutoka kundi la 201 wapo bungeni wakiwemo wale wa kundi la viongozi wa dini.
Bunge
maalum la Katiba Jumatatu saa Saba mchana lilimaliza kupokea taarifa
kutoka kamati 12 zilizokuwa zinajadili sura ya kwanza na Sita zinazohusu
muundo wa muungano kazi iliyofanywa kwa Siku Tatu.
Wakati
wa uwasilishaji wa taarifa hizo za kamati kundi la wajumbe wachache
likiongozwa na wana ukawa lilipewa masala 6 kufafanua hoja zao
zilizosomwa na wenyeviti wa kamati hizo kwa niaba yao fursa ambayo
waliitumia kueleza Maoni yao ya kukubaliana na muundo wa serikali 3
uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba.
Hoja
walizotoa ni pamoja na muungano uliopo haukuhalalishwa hususan na
serikali ya mapinduzi zanzibar, kutokuwepo kwa hati ya muungano, Mwalimu
Nyerere alitumia ujanja ujanja kutekeleza shughuli za muungano,
waliozoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi kwani wameishi kwa uongo
kwa zaidi ya miaka 50 yaani nusu karne na sasa wamefikia mwisho wake na
mengine mengi.
Jumatatu
mchana wajumbe wa bunge la Katiba walianza kuchangia kwa hoja
zilizoonyesha kuwa muungano uliodumu kwa miaka zaidi ya miaka 50 ni
halali na jana Jumanne Serikali ilitoa hati ya muungano na wajumbe hao
wa kundi la waliowengi kueleza hoja zilizotolewa na wana Ukawa za
kuwadhalilisha waasisi hazitendi haki kwa waasisi hao.
Bunge
Maalum la katiba linaloendelea hivi sasa mjini Dodoma likishindwa
kupitisha rasimu ya katiba jamhuri ya muungano wa Tanzania itaendelea
kutumia KATIBA ya zamani iliyorekebishwa Mara ya mwisho 1977.
Imeandikwa na Fakhi Karume kutoka kulee WANABIDII
No comments:
Post a Comment