Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 26 April 2014

FAIDA ZA KABICHI KWA AFYA



Kabichi

Wengi tumekuwa na mawazo mgando kuwa kabichi inafaa kwa kupikwa kama mboga na kuishia hapo.
Wapo pia wanaofahamu kuwa kabichi ni maalumu kwa ajili ya kutengeneza Salad au kachumbari inayotumika kuongeza ladha kwenye mlo.
Lakini ukweli ni kwamba kabichi ina manufaa mengi mno kiafya hasa kwa mtu anayekula mboga hii ikiwa imetayarishwa kwa kuzingatia kanuni zote za kiafya.
Vitamin K inayopatikana katika majani haya hufanya kazi kama chakula cha ubongo, kabichi husaidia kwa kiasi kikubwa mlaji kuwa na uwezo mzuri wa kufikiri.
Kwa mujibu wa jarida la Health Living kabichi ina uwezo wa kuzuia na kukabiliana na magojwa mbalimbali nyemelezi kwa ubongo.
Vilevile kabichi inatajwa kupunguza makali ya ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake. Inaelezwa kuwa tishu zilizopo ndani ya mboga hii huzuia kukua kasi ya ugonjwa wa saratani ya matiti.
Kwa wenye tatizo la kuumwa kichwa mara kwa mara supu inayotokana na kabichi iliyochemshwa ni dawa inayoweza kukabiliana na hali hiyo ndani ya muda mfupi. Kwa wale wenye ngozi yenye mafuta na kushambuliwa na chunusi sugu kabichi ina uwezo wa kukausha mafuta na kuiacha ngozi ikiwa kwenye hali ya ukavu.
Kabichi pia inatajwa kuwa kichocheo katika mzunguko wa damu na kuifanya itiririke na kuzunguka vizuri katika mishipa ya damu.
CHANZO, MWANANCHI 


No comments:

Post a Comment