Mvutano unaoendelea mashariki mwa Ukraine umesababisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi.
Rais wa Marekani Barack
Obama na viongozi wa nchi muhimu za Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya hatua
za kuiwekea Urusi vikwazo vipya. Maafisa wa Marekani wamesema vikwazo hivyo
vinaweza kutekelezwa siku chache zijazo
Afisa mmoja ambaye
hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la AFP kuwa upo
uwezekano kwamba vikwazo vipya vya Marekani vitaanza kutekelezwa Jumatatu wiki
ijayo, akionya kwamba hali nchini Ukraine inaendelea kuwa yenye wasiwasi
mkubwa.
Kansela wa Ujerumani
Angela Merkel amesema mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya
watakutana hivi karibuni kujadili vikwazo vipya vya umoja huo. Bi Merkel
ameyasema hayo baada ya mkutano kwa njia ya simu baina yake na rais Obama,
waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, rais wa Ufaransa Francois Hollande na
waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi.
''Kutokana na mkwamo
uliopo, tunapaswa kutafakari--na sio kutafakari tu, bali pia kuchukua hatua juu
ya vikwazo vipya'' amesema Angela Merkel.
Watu
binafsi na taasi ndio walengwa
Msemaji wa wizara ya
mambo ya nchi za nje ya Marekani Jen Psaki amewaambia waandishi wa habari mjini
Washington kwamba wamekuwa wakishirikiana na wenzao wa Ulaya na kwamba ni
sahihi kusema kwamba wamefika mahali ambapo suala sio kuandaa bali kuratibu
vikwazo vipya na kutafakari maamuzi yatakayofuata baadaye.
Inaelekea awamu mpya ya
vikwazo dhidi ya Warusi na waukraine wanaotuhumiwa kuendeleza hali ya ghasia,
vitawalenga watu binafsi na taasisi.
Ulaya na Marekani
zimekwishawawekea vikwazo maafisa zaid ya 10, wakiwemo viongozi wa jimbo
lililojitenga na Ukraine la Crimea.
Sekta
muhimu hazitaguswa
Akizungumza jana ziarani
Korea Kusini, Rais Obama alisema vikwazo vipya dhidi ya Urusi vilikuwa tayari,
vikisubiri tu kutekelezwa.
Hata hivyo Obama aliweka
wazi kwamba vikwazo hivyo havitazilenga sekta muhimu za uchumi wa Urusi kama
vile uchimbaji madini, nishati na sekta ya fedha. Maafisa wa Marekani wamesema
sekta hizo zitawekewa vikwazo ikiwa tu Urusi itaingiza jeshi lake ndani ya
mipaka ya Ukraine.
Tangazo
la Ikulu ya Ufaransa mjini Paris lilizungumzia pia vikwazo hivyo, likisema
viongozi wa mataifa na serikali wamezitaka nchi saba zinazoongoza kiviwanda-G7,
kuichukulia hatua Urusi bila kukawia, na kuweka uwezekano wa vikwazo vya
jumuiya ya kimataifa dhidi ya nchi hiyo.
CHANZO, VOASWAHILI
No comments:
Post a Comment