Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 12 January 2014

LIVERPOOL YAUA 5-3, SUAREZ MOTO CHINI


Nicheki: Luis Suarez akishangilia mbele ya wachezaji wenzake baada ya kufunga bao lake la pili

WASHAMBULIAJI Luis Suarez na Daniel Sturridge wamendelea kucheza vizuri pamoja wakiisaidia Liverpool kuweka rekodi ya kushinda mechi ya kwanza Uwanja wa Stoke kwa zaidi ya miaka 29 baada ya kuwalaza wenyeji, Stoke City mabao 5-3.
Suarez alifunga mabao mawili dakika za 32 na 71 na kutimiza mabao 22 katika mechi 16 za ligi na Sturridge akafunga bao lake la 12 msimu huu dakika ya 87 akicheza kwa mara ya kwanza tangu Novemba 23, mwaka jana kutokana na kuwa nje kwa maumivu ya kifundo cha mguu. 
Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Shawcross aliyejifunga dakika ya tano na Steven Gerrard dakika ya 51, wakati ya Stoke yalitiwa nyavuni na Peter Crouch dakika ya 39, Adam dakika ya 44 na Walters dakika ya 84.
Liverpool sasa inatimiza pointi 42 baada ya kucheza mechi 21 na kutulia nafasi ya nne, nyuma ya Asrenal yenye pointi 45, Chelsea 46 na Mancester City 47.  

Chanzo: Bin Zubeiry

No comments:

Post a Comment