Nicheki: Luis Suarez akishangilia mbele ya wachezaji wenzake baada ya kufunga bao lake la pili
WASHAMBULIAJI
Luis Suarez na Daniel Sturridge wamendelea kucheza vizuri pamoja
wakiisaidia Liverpool kuweka rekodi ya kushinda mechi ya kwanza Uwanja
wa Stoke kwa zaidi ya miaka 29 baada ya kuwalaza wenyeji, Stoke City
mabao 5-3.
Suarez alifunga mabao mawili dakika za 32 na 71 na kutimiza mabao 22 katika mechi 16 za ligi na Sturridge akafunga bao lake la 12 msimu huu dakika ya 87 akicheza kwa mara ya kwanza tangu Novemba 23, mwaka jana kutokana na kuwa nje kwa maumivu ya kifundo cha mguu.

Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Shawcross
aliyejifunga dakika ya tano na Steven Gerrard dakika ya 51, wakati ya
Stoke yalitiwa nyavuni na Peter Crouch dakika ya 39, Adam dakika ya 44
na Walters dakika ya 84.
Liverpool
sasa inatimiza pointi 42 baada ya kucheza mechi 21 na kutulia nafasi ya
nne, nyuma ya Asrenal yenye pointi 45, Chelsea 46 na Mancester City
47.
Chanzo: Bin Zubeiry
No comments:
Post a Comment