Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 11 December 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AWATAKA WANANCHI WATOE TAARIFA ZA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU ILI KUDHIBITI MATUKIO YA UKATILI NCHINI



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu na Wananchi pamoja na Watumishi wa Kituo cha Huduma za Sheria, mjini Unguja, Zanzibar (hawapo pichani). Masauni katika hotuba yake, alisema matukio ya unyanyasi yanaongezeka kwa wingi nchini, hivyo amewataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter na kulia ni Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji Mpatani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa anatoa hotuba yake katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu katika Kituo cha Huduma za Sheria, mjini Unguja, Zanzibar. katika hotuba yake, Masauni aliwataka wananchi nchini, kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar, Khamis Rashid Kheri baada ya kupokea Matembezi ya kupinga Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto yalioandaliwa na Baraza hilo, Mnarani Mwembe Kisonge, mjini Unguja, Zanzibar. Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na na vijana wa vikundi mbalimbali vya michezo (hawapo pichani) walivyoshiriki katika matembezi ya kupinga Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Za Binadamu. Tukio hilo liliandaliwa na Baraza la Taifa la Vijana, Zanzibar na lilifanyika Mnarani Mwembe Kisonge, mjini Unguja, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni alisema matukio ya unyanyasi yanaongezeka kwa wingi nchini, hivyo amewataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati.    Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Sehemu ya vijana ambao walishiriki Matembezi ya Kupinga Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto wakiwa wameshika bango ambalo lina ujumbe unaowataka askari kuwasaidia wananchi zaidi katika mapambano ya kudhibiti matukio ya unyanyasaji nchini. Vijana hao walipokelewa na mgeni rasmi katika tukio hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.




Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter (wapili kushoto waliokaa), Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji Mpatani (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani. Masauni alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ZLSC, mjini Unguja, Zanzibar. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment