Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 10 December 2016

MHANDISI METHEW MTIGUMWE AAPISHWA NA RAIS KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO, UVUVI NA MIFUGO

Mhandisi Mathew Mtigumwe akila kiapo mbele ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo

Na Mathias Canal

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ameamuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. 

Mhandisi Mathew Mtigumwe aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo tarehe 07 Desemba, 2016 baada ya Rais kufanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia alifanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa.
 
Uteuzi huo ulimfanya Mhandisi Methew Mtigumwe kuchukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo.Ambapo Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Katika uteuzi huo pia Dkt. Magufuli alimteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.
MWISHO

No comments:

Post a Comment