Mwenyekiti wa Tamasha la Kuombea
Amani, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 4
kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya
Kikwete. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Hamisi Pembe.
(Picha na Francis Dande)
Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI watakaoshiriki katika tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu 2015 wanaanza kuwasili Ijumaa Oktoba 3.
Aklizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 100 huku waimbaji kutoka nje ya nchi wanatarajiwa kuwasili kuanza Ijumaa.
Aliwataja waimbaji hao kuwa ni Sipho Makhabane, Solly Mahalangu (Afrika Kusini), Ephraim Sekereti (Zambia), Solomon Mukubwa (DR Congo), Sarah K (Kenya).
Aidha kutakuwa na waimbaji wadhawa akiwemo malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Bonny Mwaitege, Christopher Mwangira, John Lissu.
Kwa upande wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Kweaya ya AIC Chang'ombe na Kwaya ya St. Adrew Aglikana ya Dodoma.
Wakati huohuo Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA), limeipongeza Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwa wabunifu
wa kuinua vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili Tanzania ambao wanapata
nafasi ya kutambulika kimataifa.
Katibu Mtendaji
wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema kuwa ufanikishaji huo wa kazi za
waimbaji inayofanywa na Msama ni baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo
ufuatiliaji wa vibali vya kufanikisha tukio hilo la kuombea amani Oktoba 4.
Mngereza alisema
tamasha hilo ni lenye maana kubwa kutokana na maudhui yake, hasa ikizingatiwa
nchi inakabiliwa na Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika
Oktoba 25.
Alisema tamasha
hilo linasisitiza kuwa amani ni kitu cha msingi hasa kwa masuala ya kisiasa na
kiuchumi, ambavyo havitapata mwelekeo wake iwapo amani hiyo ikikosekana.
“Kama hakuna
amani vitu vyote havifanyiki, tamasha hilo limekuja wakati muafaka kwamba sisi
ni wamoja, Watanzania tuzingatie misingi ya amani.
“Tumekuwa ndugu
bila kubaguana kwa hali yoyote, amani tuliyopewa na Mungu, tuileee na kuitunza
tunu hiyo kwa sababu ndiyo chachu ya maendeleo yetu na taifa kwa ujumla,”
alisema.
Mkurugenzi wa
Msama Prmotions, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo
yamekamilika kwa kiasi kikubwa, hivyo alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa
wingi kufanikisha tamasha hilo.
“Nawasihi
wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili na wengine wenye mapenzi mema kwa nchi
yao, wajitokeze kwa wingi katika Uwanja wa Taifa katika tamasha la kuombea
amani Uchaguzi Mkuu,” alisema Msama.
Aidha, ametoa
shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kukubali
kubeba jahazi la tamasha hilo, kwa kukubali kuwa mgeni rasmi ambapo atatumia
tukio hilo kuwaaga mashabiki wa muziki wa Injili.
No comments:
Post a Comment