Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 21 August 2015

TANZANIA MWENYEJI FAINALI ZA U-17 AFRIKA 2019


Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Tanzania inatarajia kuwa wenyeji wa fainali za Afrika za soka kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019.
Akizungumza na BBC jana jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho la soka la Tanzania (TFF) Jamal Emmily Malinzi amethibitisha kuwa Tanzania watakuwa wenyeji wa fainali hizo .
Amesema TFF kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania walituma maombi katika shirikisho la soka la Afrika (CAF) kuomba kuwa wenyeji wa fainali hizo na hatimaye CAF imeridhia Tanzania kuwa wenyeji mashindano hayo.
Na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwa katika mikakati ya maandalizi ya fainali hizo, Rais huyo amewataka wadau mbalimbali wa soka nchini Tanzania yakiwemo mashirika ya watu binafsi , sekta binafs i kujitokeza na kutoa michango ya fedha na vifaa kwa lengo la kufanikisha fainali hizo na hatimaye kuweza kujitangaza kisoka kupitia fainali za Afrika kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment