Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 23 August 2015

PAUL MAKONDA AIPONGEZA BASATA KWA KUJALI AFYA ZA WASANII

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Paul Makonda akimkabidhi kadi ya Bima ya Afya Katibu wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Ndugu Godfrey Ndimbo. Awaliwa Ndugu Makonda alizindua semina ya siku moja kuhusu Umuhimu wa wasanii kuwa na Bima ya Afya iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Bima (NHIF) na kufanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza akisisitiza jambo wakati akiongea na Wasanii waliohudhuria semina ya Umuhimu wa Wasanii kujiwekea Bima ya Afya iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ndugu Paul Makonda.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mifuko ya Afya ya shirika hilo Ndugu Eugen Mikongoti akiongea na wasanii juu ya madhumuni ya semina hiyo ya wasanii. 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndugu Paul Makonda akiwa na viongozi wa mashirikisho ya wasanii nchini mara baada ya kuwakabidhi kadi zao za Bima ya Afya.

Msanii Bakari Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wasanii waliohudhuria semina hiyo.


Sehemu ya umati wa Wasanii waliohudhuria semina hiyo ya wasanii iliyofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA unaondelea kujengwa.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Paul Makonda amelipongeza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kujali afya za wasanii kufuatia kuandaa semina maalum kwa ajili ya kuwaelimisha wasanii umuhimu wa kuwa na bima ya afya.
Akizungumza mwishoni mwa wiki hii kwenye ufunguzi wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba, Makonda alisema kuwa pamoja na BASATA kuratibu sekta ya Sanaa limeona ni vema wasanii kulinda afya zao na kuhakikisha wanakuwa na afya njema kupitia kuwa na bima ya afya.
“Nawapongeza sana BASATA kwa kuona umuhimu wa afya kwa wasanii wetu. Kumbe pamoja na kuratibu sekta ya Sanaa na kukusanya mapato kutoka kwenye kazi za Sanaa BASATA wanauona umuhimu wa afya kwa wasanii” alisema Makonda
Aliongeza kwamba katika siku za hivi karibuni wasanii wamekuwa wakiombaomba fedha kwa ajili ya matibabu ama kutatua matatizo mbalimbali hali ambayo inatokana na wao kutojiwekea akiba ya fedha ili iweze kufaa katika kutatua changamoto hizo.
“Ni fedheha kubwa kwa wasanii tena wengine maarufu kuombaomba kwa ajili ya matibabu. Lazima watokane na aibu hii kwa kujiwekea akiba ya fedha kupitia mfuko wa Bima ya afya. Hili litamaliza kabisa tatizo la wasanii kukosa fedha za matibabu” alisema Makonda.
Aidha, Makonda alieleza kushangazwa na kukosekana kwa wasanii wengi maarufu kwenye semina hiyo na kueleza kwamba wao ndiyo wamekuwa ombaomba wakubwa pale wanapokuwa na shida ya matibabu na wengine wamefikia hatua ya kuomba hata fedha za pango.
“Nashangaa sana katika semina hii muhimu baadhi ya wasanii wakubwa siwaoni. Wanajiona wakubwa lakini wao ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuombaomba pale wanapokuwa na tatizo la matibabu na hata kodi za nyumba wanazoishi” alieleza Makonda.
Awali akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya, Katibu Mtendaji wa BASATA Ndugu Godfrey Mngereza alisema kwamba BASATA limeandaa semina hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) baada ya kuona wasanii wamekuwa na tatizo la kugharamia matibabu na wamekuwa ni wa kutembeza bakuli pale wanapougua.

No comments:

Post a Comment