Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 3 June 2015

RAFA BENITEZ ALAMBA DILI REAL MADRID

Rafa Benitez
Aliyekuwa kocha wa Napoli Rafa Benitez amethibitishwa kuwa k ocha wa Real Madrid katika kandarasi ya miaka mitatu.

Benitez mwenye umri wa miaka 55 anachukua mahala pake Carlo Ancelotti ambaye aliondoka katika kilabu hiyo miezi 12 tu baada ya kuisaidia kushinda kombe lao la kumi la vilabu bingwa Ulaya.
Benitez ambaye ni mzaliwa wa Madrid amehudumu misimu miwili kama mkufunzi wa Napoli ,baada kufanikiwa na vilabu kadhaa vya Ulaya.
Baada ya kuisaidia Valencia kushinda kombe la Uefa mwaka 2004,mwaka unaofuatia alielekea Liverpool na kuisaidia kilabu hiyo kushinda kombe la vilabu bingwa ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika kilabu hiyo ya Mersyside.
Miaka miwili baadaye aliisaidia Liverpool kufika katika fainali za kombe la vilabu bingwa Ulaya na mwaka 2013 alikuwa kaimu mkufunzi wa Chelsea waliposhinda kombe la Yuropa.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment