Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 8 May 2015

KADA WA CCM ALIYERUSHA RISASI ATOZWA FAINI 'BUKU MBILI'


Na Faustine Fabian, Mwananchi
Bariadi. Kada wa CCM Ahmed Ismail aliyerusha risasi hewani katika ofisi za Chadema wilayani Bariadi amehukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini Sh2,000 baada ya kukutwa na hatia.
Ismail alikuwa akikabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya silaha.
Mwendesha Mashtaka, Yamiko Mlekano alidai mahakamani hapo kuwa Aprili 22, mwaka huu, saa 10 jioni mshtakiwa huyo alikwenda kwenye mkutano wa hadhara wa CCM katika Mtaa wa Isanga akiwa na bastola.
Alidai kuwa siku hiyohiyo, akiwa kwenye msafara wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge alitoa silaha hiyo hadharani kisha kufyatua risasi tatu karibu  na ofisi za Chadema wilayani humo kinyume cha sheria.
Mshtakiwa alipotakiwa kujitetea kabla ya hukumu, aliomba Mahakama imuonee huruma kwa kuwa hakujua kama ilikuwa ni makosa.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Aidon Mwilapwa alitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi. Mshtakiwa huyo aliachiwa huru baada ya kulipa faini.
Ilivyokuwa
Siku ya tukio Ismail alizua taharuki baada ya kufyatua risasi tatu wakati msafara wa Chenge ulipokutana na ule wa Chadema mjini Bariadi, Simiyu.
Taharuki hiyo ilitokea katika eneo la Ofisi za Chadema Bariadi baada ya wafuasi wa chama hicho kukusanyika hapo wakitokea kwenye mkutano uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika.
Hata hivyo, taarifa za awali zilikuwa zinapingana kuhusu nani hasa aliyerusha risasi, Chadema wakidai ni Chenge na polisi wakisema ni Ismail.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment