Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 10 May 2015

CHAMA CHA UPINZANI AFRIKA KUSINI CHAMTEUA MWEUSI WA KWANZA KUKIONGOZA

Musi Maimane
Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kimemteua mwafrika kwa kwanza kukiongoza.

Wajumbe katika kongamano kwenye mji wa Port Elizabeth walimteua Musi Maimane kukiongoza chama hicho.
Bwana Maimane mwenye umri wa miaka 34 tayari anakiongoza chama hicho bungeni.
Waandishi wanadai kuwa Chama hicho cha Democratic Alliance kimekuwa kikionekana kama kinchowawakilisha watu weusi lakini sasa kinajaribu kujibadilisha ili kupata kuungwa mkono katika maeneo yote.
Hatahivyo wakosoaji wanasema kuwa Maimane hana ujuzi wa kukiongoza chama hicho.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment