Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 2 April 2015

WAWILI NMB NZEGA MBARONI KWA UPOTEVU WA MILIONI 125


Na Hastin Liumba, Nzega
WATUMISHI  wawili wa Benki  ya NMB tawi la Nzega mkoani Tabora wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za  upotevu  wa  fedha Shs. milioni  125.6.



Kamanda Bwile alisema kuwa Shaabani Andrew (40)  alisema mnamo Machi 20, 2015 katika Benk ya NMB tawi la Nzega  uligundulika upotevu wa fedha kwa njia ya mtandao zaidi ya Shs. 125,680,000 zilizopotea katika Benki hiyo.

Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la polisi lilianza uchunguzi kwa haraka na kuwatia mbaraoni watumishi wawili kwa  upotevu wa fedha  hizo huku uchunguzi wa kina unaohusisha utaalam wa fedha ukiendelea kwa kufuata miamala mbalimbali.

Bwile aliwataja watumishi hao wawili walio shikiliwa na Jeshi la polisi ni pamoja na  Sande Efrahimu (32) mfanyakazi wa NMB tawi la Nzega na Queen  Jonathan (32) mtumishi NMB tawi la Nzega.

Bwile alipoulizwa dhidi ya hatua nyingine zilizochukuliwa tofauti na hizo alisema kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo kwa kina zaidi ilikubaini jinsi zilivyopotea fedha hizo mali ya NMB.

‘’Kama jinsi nilivyo kwambia tuna washikilia hawa kwa uchunguzi na sasa tunafanya uchunguzi wa kina zaidi hasa kwa kutumia wataalam wetu ilitupate uhakika wa nani kachota pesa hizi baadae tutatoa taarifa wa vyombo vya habari kama hivi ulivyo uliza’’alisema Bwile.

Alisema wanaangalia namna fedha hizo zilivyopotea na kwamba ikibainika wamehusiaka watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment