Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 2 April 2015

WAKULIMA WA TUMBAKU WALIPWA FEDHA ZAO


Na Hastin Liumba,TaboraCHAMA cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) kimewalipa wakulima wake kiasi cha shilingi bilioni 3 kati ya bilioni 5 ambazo walikuwa wanakidai  chama hicho kwa kipindi kirefu.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mwenyekiti wa chama hicho  Mkandala  Mkandala alisema huo ni mmoja ya mikakati ya chama ya kupunguza madeni ambayo chama hicho walikuwa wanadaiwa

Alisema kwamba kupunguza deni hilo ambalo limekuwa ni kero kubwa kwao, licha ya chama hicho kuwadai wakulima kiasi cha shilingi bilioni 3.4 hatua nzuri na malengo ni kumaliza kabisa deni hilo.

Mwenyekiti huyo wa WETCU aliendelea kusema deni hilo linatokana na wakulima kudhulumiwa kutoka ndani ya vyama vyao vya msingi vya ushirika ambayo vimekuwa na watendaji ambao sio waaminifu na kuwapandikiza madeni wakulima.

Mkandala alisema kwamba kutokana na hali hiyo chama cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi  kimekusudia kutoa elimu kwa vyama vya msingi vya ushirika 90 kwa mwaka huu.

Alisema kwamba elimu hiyo ambayo itakuwa msingi kwa wakulima wa tumbaku kupata elimu ambayo itavijenga vyama hivyo ili kuweza kuondokana na matatizo ambayo waliyapata kipindi cha nyuma.

Alisema kwamba elimu hiyo itatolewa kwa awamu kwa kuanzia na vyama 90 mwaka huu  na kuendelea hadi  kuvifikia vyama vyote 217 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Alisema kwamba elimu hiyo itawahusisha viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika  ambao ni mwenyekiti ,Katibu Meneja na mhasibu wa chama husika.

No comments:

Post a Comment