Pages

Pages

Pages

Friday 13 March 2015

UNYANYAPAA WADAIWA KUKIMBIZA WENYE VVU HOSPITALI


Na Hastin Liumba,Tabora
HALI ya Unyanyapaa miongoni mwa jamii kumesababisha baadhi ya wagonjwa wa maambukizi ya VVU kujificha na kukatisha tiba hali inayopelekea wengi wao kupoteza maisha, imeelezwa.

Sara Kabeya muuguzi katika hospitali ya St Anna Misheni Ipuli alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari na ujumbe toka EGPAF.

Hatua hiyo ilikuja kufuatia ujumbe ulioongozwa na Mratibu mawasiliano Mercy Nyanda toka makao makuu ya shirika lisilo la kiserikali la EGPAF linalopata ufadhili toka CDC na USAID nchini Marekani.

Kabeya alisema unyanyapaa bado ni tatizo kubwa miongoni mwa jamii hali ambayo inakuwa tatizo kubwa kwao kama watoa huduma kwa wajawazito na watoto wenye VVU.

Muuguzi huyo alisema baadhi ya wagonjwa wakianza tiba hukatisha kurejea tena kwenye huduma na hiyo hutokana na hali ya Unyanyapaa hivyo wengine hupoteza maisha kwa kukosa huduma.

“Baadhi ya wagonjwa hutoka wilayani kama vile hospitali zingine au Igunga na kuja hapa kwetu….ni jinsi gani bado elimu ya unyanyapaa inapaswa kuedelea kutolewa vinginevyo hali itazidi kuwa mbaya”.alisema.

Kabeya anasema licha ya kuwepo kwa hali hiyo bado ushiriki wa wanaume kuja vituo vya kutolea huduma na tiba ni mdogo na mara nyingi wanawake wajawazito hufikia mahali wanadanganya waume zao wamefariki.

Aidha alibainisha mara kadhaa imejitokeza mume na mke wanafichana kama wameambukizwa VVU hilo nalo ni tatizo kubwa kwenye jamii yetu.

Kuhusu hali ya maambukizi Kabeya anasema bado yako juu hivyo ni juhudi zinahitajika ili kuweza kukabiliana na hali hii.

Akizungumzia vifaa tiba Kabeya alisema vipo kwa wastani japokuwa ipo haja kukabiliana na upungufu uliopo japo si mkubwa sana.

Mercy Nyanda Mratibu mawasiliano wa shirika lisilo la kiserikali la EGPAF  awali alisema kinamama wengi wamekuwa wakijificha kuja kwenye vituo vya kutolea huduma na tiba hali inayosababisha wengi wao kujifungua watoto wenye VVU.

Nyanda alisema shirika la EGPAF limeanza kuchukua hatua kushughulikia tatizo hilo kuokoa wajawazito  na watoto wenye VVU na kuokoa watoto ambao watakingwa wasiambukizwe.

No comments:

Post a Comment