Pages

Pages

Pages

Saturday 14 March 2015

AL SHABAAB WACHUKUA MWILI WA KIONGOZI WAO

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Shabaab

Taarifa kutoka Somalia zinasema kundi la kigaidi la Al Shabaab limeuchukua mwili wa kiongozi wao anayedaiwa kuuwawa na kombora la Marekani.

Kiongozi huyo, Adan Garar, anadaiwa kuwa mojawapo ya waliopanga shambulio la Westgate Mall,jumba la kibiashara katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, ambapo zaidi ya watu sitini na saba waliuawa.
Adan Garar ameripotiwa kuuwawa akiwa ndani ya gari siku ya alhamisi, kwenye shambulio hilo lililotekelezwa na Marekani.
Watu wengine wawili waliokuwa wakisafiri naye pia wameuawa.
Garar alishukiwa kuandaa shambulizi la kigaidi kwenye jumba la Westgate mnamo mwaka wa 2013, ambapo watu sitini na saba waliangamia.
Aidha taarifa zingine zinasema Garar alikuwa akipanga mashambulio sambamba katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya, ambapo Polisi wa kupambana na ugaidi walinasa gari moja ambalo lilikuwa limejaa vilipuzi, ambavyo, wanasema vilikuwa vikilengwa kwenye maeneo ya watu wengi.
Kundi la Al shabaab limekuwa likitekeleza mashambulio ya kigaidi ndani ya Kenya kutokana na wanachokitaja kama kulipiza kisasi dhidi ya mashambulio ya vikosi ya Kenya chini ya mwamvuli wa Amisom, kikosi cha Umoja wa Afrika kinacholinda amani Somalia.
Marekani imetumia makombora mara kadhaa kuwalenga makamanda wa Al Shabaab ndani ya Somalia.
Ni katika shambulio kama hili ambapo aliyekuwa kiongozi mkuu wa AL Shabaab, Ali Godane aliuwawa Septemba mwaka uliopita .
Vilevile kumekuwa na mashambulio mengine mengi ambayo yamedaiwa kulenga kambi za kundi hilo, bila thibitisho lolote.
CREDIT SOURCE: BBC

No comments:

Post a Comment