Pages

Pages

Pages

Saturday 14 March 2015

UNENE WAMFANYA KUKOSA BURUDANI UINGEREZA

Klabu ya burudani nchini Uingereza

Mama mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake wawili walizuiliwa kuingia katika kilabu moja ya burudani kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni wanene sana na wenye sura mbaya.

Stacey Owen 33, alikuwa ametoka na marafiki zake wawili kwa ajili ya kupata burudani wakati wa usiku siku ya jumamosi alipokataliwa kuingia katika baa moja jijini Manchester kwa sababu ya unene wake.
Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine wakiingia katika baa hiyo maarufu mjini humo,
Klabu ya burudani Uingereza
Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na wamiliki wa Baa hiyo lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka kwao.
Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni mrembo sana lakini kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa wateja.
CREDIT SOURCE: BBC

No comments:

Post a Comment