Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 1 January 2015

IRINGA WANAKULA HATA PUNDA!

 Jamani hala hala mti na macho! Nyie mlio waroho wa nyamahasa muwapo safarini. Siyo kila nyama choma ni ya ng'ombe au mbuzi, mnapaswa kuwa makini. Tazama huyu bwana aliyeuficha uso wake ambaye ni mkazi wa Izazi wilayani Iringa anachokifanya. 

Jamaa aliukuta mzoga wa punda, ambaye hajulikani alikufa kwa ugonjwa gani, yeye akaanza kumchuna kama picha zinavyoonyesha. Baada ya hapo akabeba nyama na kuisambaza anakokujua mwenyewe. Ukikutana nayo imechomwa hutakuwa na muda wa kuuliza, utaibugia tu! Kazi kwenu.
Lakini naambiwa kwamba mikoa kadhaa ikiwemo Singida na Dodoma hivi sasa wanakula nyama ya punda, na sasa idadi imeongeza - Iringa nayo imo.

No comments:

Post a Comment