Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 1 January 2015

HAPPY BIRTHDAY: MZEE WA MCHINGA, JACK WILSHERE NA COLIN MORGAN

MUDHIHIR MOHAMMED MUDHIHIR
Mbunge wa zamani wa Mchinga. Elimu ya msingi aliipata katika shule za Mchinga (1958 hadi 1959), Msinjahili (1959 hadi 1961) na Mangamba Middle School (1962 hadi 1965) kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Lindi (1966 hadi 1969). Baadaye akajiunga na Chuo cha Ualimu Marangu kwa mafunzo ya Cheti cha Ualimu Daraja A (1973 hadi 1974). Kati ya mwaka 1981 na 1982 alisoma kidato cha tano na sita katika shule ya Kujitegemea (Private School). Mwaka 1988 na 1989 alihitimu Cheti cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 2000 alijiunga na masomo ya shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Washington, Marekani lakini hakumaliza.

Kati ya mwaka 1970 na 1973 alikuwa Msaizidi wa Usajili katika Wizara ya Elimu. Mwaka 1975 hadi 1981 alikuwa Mwalimu Daraja la Tatu A. Kuanzia mwaka 1981 hadi 1995 alikuwa Ofisa Usalama wa Taifa, kipindi ambacho pia alikuwa Mkuu wa Chuo cha Usalama wa Taifa cha Zanzibar. Mwaka 1997 hadi 2005 alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo.
Alikuwa anamiliki bendi yake ya muziki wa dansi ya Mchinga Sound, lakini ikamshinda kuiendesha.

JOHN SULLIVAN 
John Sullivan (John A. Sullivan) alizaliwa Ijumaa, Januari 01, 1965 mjini Tulsa, Oklahoma nchini Mrekani. Ni mwanasiasa maarufu Mkatoliki huko Marekani. Baba yake ni Daniel na mama yake ni Mag. Kwa kuzaliwa Januari Mosi, nyota yake ni Mbuzi (Capricon).
John Sullivan alisoma katika shule ya Bishop Kelley High School, Tulsa, Oklahoma na akapata shahada yake ya kwanza ya utawala katika biashara (BBA) katika Chuo Kikuu cha Northeastern State University, Tahlequah, Oklahoma mwaka 1992.
Mkewe anaitwa Judy Beck.


COLIN MORGAN

Mwigizaji huyu wa runinga alizaliwa Januari Mosi, 1986 huko Ireland Kaskazini na nyota yake ni Mbuzi (Capricon).
Kwa wafuatiliaji wa tamthiliya za runinga, lazima wanamfahamu Colin Morgan, kijana aliyejipatia umaarufu mkubwa kwenye tamthiliya ya Merlin iliyokuwa ikirushwa na BBC.
Kabla ya kuwa maarufu alisoma shule ya muziki na maigizo ya Royal Scottish Academy. Ameshiriki filamu za Island (2011) na Parked (2010). Kaka yake anaitwa Neil.

MORRIS CHESTNUT

Staa huyu wa maigizo ya runinga alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1969 huko California.
Anafahamika zaidi kutokana na ushiriki wake katika filamu iliyoteuliwa kuwania tuzo za Oscar ya Boyz in the Hood, ambapo alishiriki kama Visitor Ryan.
Wakati akiwa chuo alikuwa mwanachama wa Phi Beta Sigma.alimuoa Pam Byse mwaka 1995. Ameshiriki pia filamu ya Under Siege 2: Dark Territory akiwa na Steven Seagal, na filamu yake ya kutisha ya Half Past Dead.

 

JACK WILSHERE

Mchezaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya England ambaye alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1992. Ametimiza miaka 23.

Wilshere alijiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2008 na mwaka 2010 akaitwa kwenye timu ya taifa ya England. Wakati anajiunga na ‘Wapiga Bunduki wa London, alitokea kwenye timu ya vijana (Academy) ambako alijiunga tangu akiwa na miaka 9.

Alianza kuiwakilisha England akichezea timu zenye umri mkubwa kuliko yeye, ambapo aliitwa kwenye timu ya U16 akiwa na miaka 14, na baadaye kwenye timu ya U17 akiwa na miaka 15.

Mwaka 2011 alipata mtoto wa kiume, aitwaye Archie Jack Wilshere.

 

 

TANK

Mwanamuziki wa Marekani, mzaliwa wa Wisconsin tarehe kama ya leo mwaka 1976 leo ametimiza miaka 39. Mwimbaji huyu na mtayarishaji wa muziki wa R&B amepata kuwania Tuzo za Grammy na ametoa albamu nyingi ikiwemo Now or Never. Pia ametoa single kama "Emergency" na "Sex Music."
Kabla ya kuingia kwenye muziki alikuwa mchezaji wa kandanda la Kimarekani na alipata ofa nyingi za kucheza kwenye timu za vyuo lakini akazitosa na kuingia kwenye muziki. Alitoa albamu ya Sex, Love, & Pain, ambayo iliingia kuwania Tuzo za Grammy katika Albamu Bora ya R&B mwaka 2008.
Watoto wake ni Jordan, Ryen, Zoey, na Durrell Jr. Alirekodi wimbo wa "Take My Time" akishirikiana na Chris Brown.

 

SOPHIE OKONEDO

Mwigizaji wa filamu aliyezaliwa nchini Uingereza mwaka 1968. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na ushiriki wake katika filamu ya Hotel Rwanda mwaka 2005 na The Secret Lives of Bees mwaka 2008. Ushiriki wake katika filamu ya Tsunami: The Aftermath ulimfanya ateuliwe kuwania Tuzo za Golden Globe. Alisoma katika Chuo cha Sanaa za Maigizo cha Royal Academy kabla ya kupata fursa ya kuingiza vipindi vya televisheni kwenye kituo cha BBC. Aliteuliwa kuwania Tuzo za Academy kwa ushiriki wake kwenye filamu ya Hotel Rwanda.
Ana binti mmoja, Aoife, aliyezaa na mpenzi wake wa zamani Eoin Martin. Aliigiza kama May Boatwright akishirikiana na Queen Latifah katika filamu ya mwaka 2008, The Secret Life of Bees.

 

J. EDGAR HOOVER

Mkurugenzi huyu wa zamani na wa kwanza wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1895 na akafariki Mei 2, 1972 akiwa na miaka 77. Alikuwa Mkurugenzi wa FBI kati ya mwaka 1935 hadi 1972 na ndiye mkurugenzi wa shirika hilo aliyekaa kwa miaka mingi zaidi (37). Yeye ndiye aliyeanzisha utaratibu wa kumbukumbu za alama za vidole na na maabara za uchunguzi (forensic laboratories).
Alikuwa mwimbaji mzuri wa kwaya ya shule, mshiriki wa timu ya midahalo, ofisa wa akiba wa jeshi tangu akiwa shule ya sekondari. Alitumia FBI kuwatisha wanasiasa na wanaharakati na kutoa mafaili ya siri kwa wanasiasa. Huyu ndiye aliyemsaliti Martin Luther King Jr. kwa sababu aliamini kwamba mwanaharakati huyo alikuwa anahatarisha usalama wa Marekani.
Baba yake mkubwa alikuwa balozi wa heshima wa Uswisi nchini Marekani. Alikuwa Mkurugenzi wa Kwanza wa FBI akiwa chini ya Rais Franklin D. Roosevelt na kumalizia chini ya Rais Richard Nixon.

 

 

DIAMOND WHITE

Mwanamuziki huyu aliyezaliwa tarehe kama ya leo huko California, Marekani mwaka 1999 anatimiza miaka 20. Ni maarufu katika muziki wa R&B na pop na alimaliza akiwa wa tano katika awamu ya pili ya kipindi cha "The X-Factor".
Alichaguliwa katika utengenezaji wa kipindi cha "The Color Purple" tangu akiwa na miaka nane na alishiriki kwenye ziara ya taifa. Sauti yake ilitumika katika vipindi vya "Transformers: Rescue Bots" na "Phineas and Ferb" kupitia Chaneli ya Disney.

Yeye na mama yake walihangaika kiuchumi wakati alipokuwa anaanza maisha ya muziki, wakati mwingine akilala kwenye kochi kwenye kibanda tu. Wakati akiwa katika kipindi cha "The X Factor" alikuwa chini ya uangalizi wa Britney Spears.

No comments:

Post a Comment