Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 10 December 2014

TABORA IKO NYUMA MATUMIZI YA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO

Na Hastin Liumba, BrotherDanny5 Blog
Tabora: MKOA wa Tabora umefikia kiwango cha asilimia 19 za utumiaji huduma za uzazi wa mpango ikiwa ni kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na mkoa wa Kilimanjaro ambao wamefikia hatua ya asilimia 50 za huduma hiyo, imeelezwa.

Ofisa utekelezaji wa mpango wa huduma za uzazi wa mpango Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Isabela Nyakusi alisema hayo wakati akisoma taarifa yake kwa wananchi katika uzinduzi wa huduma hiyo Kanda ya Magharibi kwa Mkoa wa Tabora.
Nyalusi alisema mkoa wa Tabora kiwango hicho bado ni kidogo mno hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kufanyika kufikia malengo.
Kutokana na hali hiyo Wizara imeamua kujipanga upya na kusukuma zaidi nguvu katika kutilia mkazo na kusadiana na viongozi wa mikoa ya kanda hizi za Ziwa na Kanda ya Magharibi katika kuongeza kiwango cha utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango.
Nyalusi alisema katika kujipanga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kuandaa mpango kazi wa kusukuma kwa kasi jitihada za kuongeza kiwango na wigo wa utoaji huduma hizo kwa wananchi.
Alisema mpango huo ulizinduliwa mwezi mei 15 mwaka huu na Rais Dk. Jakaya Kikwete ambaye alisisitiza umuhimu wa wa kila mmoja wetu,viongozi,watendaji na wafanya maamuzi katika ngazi zote kuwajibika zaidi katika kuongeza kiwango cha utumiaji huduma hizi.
Alisema hali hiyo itasadia zaidi kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto.
Aidha afisa huyo alisema wamejipanga kuhakikisha mikoa hii ambayo kiwango chake kiko chini zaidi katika matumizi ya huduma hizi wataongeza jitihada zaidi ili kupanua wigo na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Alisema ili kuwafikia watu wengi zaidi wanaohitaji huduma hizi anaamini jitihada ikifanyika mafanikio yatapatikana.
Alisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inathamini zaidi kwa kiwango kikubwa kutoa kipaumbele kwa suala zima la kuongeza wigo wa utolewaji wa huduma za uzazi wa mpango kwa lengo la kuhakikisha zinawafikia wananchi wote nchini wahitajio huduma hizi.
Alisema Wizara iliandaa na kuzindua mango mkakati wa kitaifa wa uzazi wa mpango uliothaminiwa (Family Planning Costed Iplementation Programme).
Alibainisha mapango huo ulizinduliwa mnamo mwezi machi 2010 unalenga katika kufikia katika kuongeza kasi ya kuinua kiwango cha utumiaji wa njia za kisasa  za uzazi wa mpango kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 27 na kufikia lengo la asilimia 60.
Alibanisha mambo mbayo yatasadia yaliwekwa ni kuhakikisha upatikanaji huduma za kisasa za uzazi wa mpango,kuongeza kasi ya utoaji huduma,kuboresha huduma na utunzaji wa kumbukumbu zihusuzo huduma za uzazi wa mpango.

No comments:

Post a Comment