Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 1 November 2014

WANAJESHI BURKINA FASO WAMUUNGA MKONO KANALI ISAAC ZIDA BADALA YA JENERALI TRAORE

Kanali Zida akihojiwa na wanahabari mda mfupi baada ya kutangaza kwamba amechukua mamlaka
Viongozi wa jeshi nchini Burkina Faso wamemuunga mkono Kanali Issac Zida kama kiongozi wa serikali ya mpito nchini humo.

Taarifa hiyo inaonekana kumaliza tofauti kuhusu ni nani aliyemrithi Rais Blaise Campaore ambaye alijiuzulu kufuatia maandamano ya kumpinga.
Luteni kanali Zida alitoa hotuba yake katika runinga usiku kucha ili kutangaza kwamba anachukua mamlaka.
Hatua hiyo inaonekana kutofautiana na ile ya mkuu wa jeshi Jenerali Honore Traore ambaye alijitangaza kuwa kiongozi mpya mda mfupi baada ya kujiuzulu kwa Campaore.
Hatahivyo Sahihi ya Jenerali Honore Traore ilikuwa katika taarifa iliosomwa na Luteni kanali Issac Zida ambaye inadaiwa alichaguliwa na wakuu wote wa jeshi kuongoza.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment