Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 17 November 2014

WAANDAMANA KUPINGA KUVULIWA NGUO

Maandamano makubwa yaliyopewa kauli mbiu ya 'My dress My choice'

Wanawake mjini Nairobi, Kenya leo wameandamana kupinga kitendo cha mwanamke mmoja kuvuliwa nguo wiki jana kwa madai kuwa alikuwa amevalia sketi fupi sana.

Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo zake na wanaume katika kituo cha magari ya abiria kati kati mwa Nairobi.
Na wanaume walikuwemo kuwaunga mkono wanawake katika maandamano hayo
Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke yanamhusu nini mwanamume ambaye sio mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima, basi na wanaume wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavuliwe nguzo zao.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment