Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 1 November 2014

TANZANIA KUTUMIA JOTO ARDHI KUPUNGUZA TATIZO LA UKOSEFU WA NISHATI

Ziwa Magadi

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

Arusha: TANZANIA inatarajia kutumia nishati ya joto ardhi ambapo nishati hiyo itaweza kusaidia maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya Viwanda pamoja na kilimo ambapo pia nishati hiyo itakuwa ni ya kudumu.

hataivyo uwepo wa nishati joto hiyo hapa nchini utaweza kuruhusu uzalishaji kuongezeka kwa kasi tofauti na sasa ambapo wakati mwingine shuguli za kila siku zina simama kutokana na ukosefu wa nishati mbadala.
kauli hiyo imetolewa na Naibu Kamisha wa Nishati mbadala Edward Ishengoma wakati akiongea na wadau wa joto ardhi ambao wanapewa mafunzo pamoja na mbinu mbalimbali za kitaalamu za joto ardhi.
Ishengoma alisema kuwa uzoefu kwa nchi ambazo zimeshaanza kutumia nishati hiyo ya joto ardhi unaonesha kuwa wameweza kupiga hatua sana kwenye masuala ya maendeleo na hivyo basi kama Tanzania itatumia nishati hiyo  nayo itaweza kukua kiuchumi kwani kazi nyingi za uzalishaji zinategemea sana Nishati.
Alitaja nchi ambazo mpaka sasa zimeshatumia Nishati hiyo ya Joto ardhi kuwa ni nchi ya Ethiopia, pamoja na nchi ya kenya na hivyo sasa nayo Tanzania itaaanza kutumia nishati hiyo ambayo tafiti zimeonesha kuwa nishati hiyo ipo.
Aliongeza kuwa uwepo wa nishati hiyo hapa nchini utaweza kusaidia hata kuongezeka kwa mambo mbalimbali hususani kwenye sekta ya uchumi, lakini pia hata kwa wawekezaji ambao nao wataweza kufanya kazi zao kwa kuwa nishati itakuwepo itakuwa ni ya kudumu kwani nishati hiyo ikishawekwa imeweka na haikatiki ovyo kwani wakati wa uwekaji watatumia bomba la urefu wa kilomita mbili na nusu hadi tatu kwenda kwenye miamba tofauti na nishati nyingine.
"Nishati ndio kila kitu hapa nchini sasa uwepo wa nishati hii utasaidia sana tanzania kuweza kupanuka zaidi na sisi tunachokitaka ni kuwa watanzania sasa wajue kuwa kuna kitu kama hiki lakini pia waweze kujua kuwa nchi yetu imepita katika bonde la Afrika ya Mashariki kwa hiyo lazima tutanufaika," aliongeza Ishengoma.
Awali Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela aliongeza kuwa Serikali ina mkazo mkubwa sana wa kuendeleza nishati kwa Watanzania kwani tafiti zinaoenesha kuwa ili umaskini uweze kutoweka ni lazima kuwepo na nishati.
Mbali na hayo Mongela alisema kuwa nishati hiyo ya joto ardhi ipo sehemu nyingi mfano katika maeneo ya Engaruka, lakini pia katika eneo la Natron hivyo basi kuna umuhimu wa sekta husika kuhakikisha kuwa wanajifunza kwenye kama Kenya, lakini pia Ethiopia ambazo tayari wameshatumia teknolojia ya joto ardhi.

No comments:

Post a Comment