Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 5 November 2014

SUDAN KUSINI YAKUMBWA NA VIKWAZO

Rais Salva Kiir na Riek Machar waliposaini makubaliano ya amani
Marekani imesema itapeleka rasimu ya maazimio ndani ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo dhidi ya watu wanaozorotesha hali ya kisiasa nchini Sudan Kusini.

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia amesema baadhi ya wanachama wa baraza hilo wanaunga mkono hatua ya kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara ya silaha.
Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa.
Mapigano yameendelea nchini Sudan Kusini, ingawa kumekuwa na jitihada za kimataifa kuhakikisha makubaliano ya amani yanatekelezeka.
Mzozo wa kuwania madaraka uliokuwepo kwa miezi kumi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar umegharimu maisha ya maelfu ya Watu na takriban watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao.
Makubaliano ya amani yaliyotiwa saini yalishindwa, kwa kuwa pande zinazokinzana zilishindwa kuunda Serikali ya umoja.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment