Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 7 November 2014

RAIS MASKINI ZAIDI DUNIANI APEWA DOLA MILIONI MOJA AUZE GARI LAKE LA VOLKSWAGEN BEETTLE

Rais Jose Mujika na mkewe ndani ya gari lao la Vokswagen. Rais huyo wa Uruguay ndiye rais masikini zaidi na amepewa dola millioni 1.
Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema kuwa amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari lake aina ya Volkswagen.
Bwana Mujica, aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake ,alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu katika eneo la uarabuni.
Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais Mujika ambaye anajulikana kama Pepe anaishi katika shamba lake na hutoa pato lake kwa watu masikini.
Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari lake la Volkswagen
Busqueda liliripoti kwamba ombi la gari hilo lilifanywa katika mkutano wa kimataifa mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz Bolivia.
''Nilishangaa mara ya kwanza ,a hivyobasi nikapuzilia mbali.lakini baadaye ombi jengine lilikuja na hivyobasi nikaanza kulichukulia kuwa swala la umuhimu'',. Alisema Mujika.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment