Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 10 November 2014

MAJUU HAMNAZO: JAMAA ATENGENEZA GARI INAYOTEMBEA CHINI-JUU!

Tazama video ya gari hiyo ya ajabu. 
 Sullivan akitanua na gari lake la ajabu ambalo linaonekana likitembea chini-juu. (Imetayarishwa na brotherdanny5.blogspot.com kwa msaada wa mashirika).

Kuna watu wengine wamepinda, lakini wengine wamenyongorota kabisa! Fundi makenika mmoja wa jijini Illinois, Marekani, Rick Sullivan ametoa kali ya mwaka.

Jamaa huyo ambaye amekuwa akikarabati magari yaliyopata ajali, hivi karibuni aliamua kukarabati gari moja lililopata ajali na sasa linaonekana kama liko chini-juu.
Sullivan alitumia miezi sita na Dola 6,000 (takriban Shs. 9.6 milioni) kutengeneza gari hilo kwa kuunganisha vipande vya magari mawili tofauti: Ford Ranger pick-up iliyotengenezwa mwaka 1991 na Ford F-150 pick-up iliyotengenezwa mwaka 1995 ambayo ilikaa juu pamoja na magurudumu yake yanayozunguka.
Sullivan alipata wazo hilo wakati alipoitwa kwenda kuikokota Ford Ranger iliyopinduka chini-juu na kuipeleka kwenye gereji yake.
 Sullivan akiendelea na ukarabati wa gari lake la ajabu

"Nilitengeneza gari hili kwa kukusanya vipande vya Ford F150, tulinunua vipande tofauti sehemu mbalimbali," aliiambia Barcroft TV. "Hakuna alama rasmi. Nilianza tu kununua vipande na kuviunganisha pamoja. Yote yalikuwa mawazo yangu na tulilazimika kufanya marekebisho kila mahali, lakini ilionekana kana kwamba nililibuni."
Hivi sasa Sullivan amekuwa akivuta makundi ya watu kumtazama kila anapopita na gari hilo mjini Clinton, Illinois.
"Watu wanastaajabu," alisema, kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail. "Ni moja ya mambo yale yanayoonekana kwa mara ya kwanza, ni vigumu kutambua mara unapolitazama lakini ukiangalia kwa mara ya pili utakuta kila mmoja anataka asogee karibu kulitazama."
Wakati mwingine mshangao huo unamfanya aogope, ambapo siku moja kundi la maofisa wa polisi walilazimika kumfuatilia mjini DeQuoin, Illinois.
"Waligeuza wakati nilipokutana nao na kuanza kunifukuzia. Watu waliokuwa pembeni wakaanza kuwazomea," aliuambia mtandao wa Pantagraph.com. "Kisha polisi hao wakachukua simu zao za mikononi na kuanza kupiga picha na mambo yakawa shwari."


No comments:

Post a Comment